WFP yawasilisha msaada wa China kwa Waafghanistan 70,000 wasio na chakula (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2023
WFP yawasilisha msaada wa China kwa Waafghanistan 70,000 wasio na chakula
Mfanyakazi akipakia chakula cha msaada kutoka China kwenye lori ndani ya ghala huko Kabul, Afghanistan, Julai 17, 2023. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)

KABUL - Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Afghanistan limesema Jumatatu kwamba limeanza kusambaza kwa wenyeji shehena ya chakula cha msaada kutoka China.

Kwa mujibu wa WFP, msaada huo wa chakula, ukiwemo unga wa ngano, mbaazi za njano, mafuta ya mboga na chumvi, unatarajiwa kusaidia wakazi 70,000 maskini wa Afghanistan kwa muda wa miezi miwili katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita.

WFP Afghanistan inakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa ufadhili mwaka huu, na msaada huu wa China "umekuja katika wakati muafaka," amesema Liu Xuerong, mkuu wa Shirika la WFP Afghanistan, huku akiongeza kuwa shirika hilo linakaribisha aina yoyote ya misaada, ama kwa utoaji vitu au kwa pesa taslimu, na liko tayari kuendeleza ushirikiano na serikali ya China katika nyanja zaidi, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa watu wenye ujuzi wa kilimo.

"China itaendelea kushirikiana na WFP kutoa msaada wa chakula kwa watu wa Afghanistan kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kusini-Kusini," amesema Balozi wa China nchini Afghanistan Wang Yu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya WFP kuhusu hali ya Afghanistan iliyotolewa Mwezi Juni, watu milioni 15.3 nchini Afghanistan wanakadiriwa kuwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula kati ya Mei na Oktoba 2023.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha