Mpango wa mafunzo unaofadhiliwa na China wawawezesha madereva vijana wa treni nchini Ethiopia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2023
Mpango wa mafunzo unaofadhiliwa na China wawawezesha madereva vijana wa treni nchini Ethiopia
Dejen Gezu, mmoja wa madereva wa kwanza wenye leseni ya kuendesha treni zinazotumia nishati ya umeme nchini Ethiopia, akifanya kazi ndani ya treni katika Stesheni ya Indode ya Reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti mjini Addis Ababa, Ethiopia, Julai 13, 2023. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

ADDIS ABABA - Dejen Gezu, mmoja wa madereva wa kwanza wenye leseni ya kuendesha treni zinazotumia nishati ya umeme nchini Ethiopia, amepewa majukumu mawili ya kuendesha kwa usalama reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti iliyojengwa na China na kutoa mafunzo kwa madereva vijana.

Gezu anajieleza kama mfano wa mafanikio ya uhamishaji maarifa na uzoefu wa China katika kusaidia azma ya Ethiopia ya maendeleo na kufikia mambo ya kisasa.

"Nilikuwa tu mkufunzi wa udereva wa treni, na nilifunzwa na Wachina. Sasa, natoa mafunzo kwa wakufunzi wengine. Sasa tunaweza kutoa mafunzo kwa kutumia wataalam wetu wenyewe," Gezu amesema. Amepongeza uungaji mkono wa China kwa Ethiopia kutoka katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya reli hadi kuwawezesha wenyeji kupata maarifa na ujuzi wa uendeshaji wa reli.

Gezu ni mmoja wa wahitimu watatu bora wa programu iliyofadhiliwa na serikali ya China ambayo ilitoa kozi kwa Waethiopia takribani 34 juu ya kuendesha treni zinazotumia nishati ya umeme.

Sasa akiwafundisha vijana wenzake wa Ethiopia kile alichojifunza nchini China, Gezu anazungumzia sana kuhusu ushiriki wa Wachina nchini Ethiopia, kwa shauku na kuvutiwa na mpango wa China wa kujenga uwezo nchini Ethiopia.

Reli ya Ethiopia-Djibouti yenye urefu wa kilomita 752, ambayo pia inajulikana kama reli ya Addis Ababa-Djibouti, ni reli ya kwanza ya kutumia nishati ya umeme inayovuka mpaka barani Afrika, mradi ambao ni muhimu chini ya mfumo wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililopendekezwa na China.

Abdi Zenebe, afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti (EDR), amesema mpango huo wa kuwajengea uwezo wenyeji umekuwa ukiendelea tangu kuanza kuendeshwa kwa reli hiyo.

"Mchango wa uhamishaji ujuzi ni muhimu sana, hasa kwetu, ambao tuko mwishoni mwa mnyororo wa kupokea matunda." Zenebe ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni.

Hadi sasa, reli ya Ethiopia-Djibouti imetoa nafasi 55,000 za ajira nchini Ethiopia na Djibouti na kutoa fursa za mafunzo kwa watu wenye ujuzi zaidi ya 3,000, na kuweka msingi thabiti wa maendeleo ya sekta ya reli katika nchi hizo mbili, kwa mujibu wa serikali ya Ethiopia.

Wafanyakazi wenyeji wanachukua zaidi ya asilimia 90 ya wafanyakazi wote wanaotoa huduma za abiria na mizigo.

Reli hiyo imeshuhudia safari 1,824 za treni za abiria zilizobeba watu karibu 530,900 na safari 6,133 za treni za mizigo zikiwa zimeshabeba mizigo yenye uzito wa takriban tani 7,328,500 za bidhaa tangu ilipoanza kufanya kazi Januari 2018, kwa mujibu wa takwimu rasmi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha