Jeshi la Anga la China kuajiri makadeti bora zaidi kuwahi kutokea Mwaka 2023 (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2023
Jeshi la Anga la China kuajiri makadeti bora zaidi kuwahi kutokea Mwaka 2023
Makadeti wa Jeshi la Anga la China wakishiriki katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kuwasili kwenye Chuo Kikuu cha Anga cha Jeshi la Anga la China, Julai 19, 2023. (Picha na Yu Hongchun/Xinhua)

BEIJING - Idara ya kuajiri ya jeshi la anga la China imesema Jumatano kwamba, idadi ya makadeti wa Jeshi la Anga la China wanaoajiriwa mwaka huu inavunja rekodi na uwezo wao vimefikia viwango vipya, idara ya uajiri wa jeshi hilo imesema Jumatano.

Idadi ya makadeti waliokidhi kiwango cha marubani wa kivita imeongezeka sana, na asilimia 95 ya makadeti hao wana uwezo mkubwa wa kurusha ndege, idara hiyo imesema.

Jeshi la Anga la China limehusisha maendeleo yake ya uajiri na utangazaji kwa umma wa kina, mifumo iliyoboreshwa ya uteuzi na tathmini, na ushirikiano kati yake na vyuo vikuu vya kiraia.

Ili kuongeza hisia zao za kujivunia, makadeti hao wapya watasafirishwa kwa ndege ya usafiri ya Y-20 siku ya Jumatano na Alhamisi kutoka miji mitano kote nchini China hadi Chuo Kikuu cha Anga cha Jeshi la Anga la China huko Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha