Mtambo wa kwanza duniani wa kuzalisha umeme kwa upepo baharini wa 16 MW waanza kufanya kazi huko Fuzhou, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2023
Mtambo wa kwanza duniani wa kuzalisha umeme kwa upepo baharini wa 16 MW waanza kufanya kazi huko Fuzhou, China
Picha hii ya angani iliyopigwa Juni 28, 2023 ikionyesha mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 16 kwa upepo uliofungwa kwenye shamba la kuvuna upepo baharini la Fujian linaloendeshwa na Shirika la China Three Gorges karibu na pwani ya Mkoa wa Fujian Kusini Mashariki mwa China. (China Three Gorges Corporation/ Xinhua)

FUZHOU - Mtambo mkubwa wa kwanza duniani wa kuzalisha umeme kwa upepo baharini wenye uwezo wa megawati 16 kwenye pwani ya Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China umeunganishwa kwa mafanikio kwenye gridi ya taifa ya China na kuanza rasmi kuzalisha umeme siku ya Jumatano.

Mtambo huo ulioko kwenye shamba la kuvuna upepo baharini la Fujian, ambalo linaendeshwa na Shirika la China Magenge Matatu (Three Gorges), una uwezo mkubwa zaidi wa kitengo kimoja cha kuzalisha umeme kwa kulinganisha na mitambo yote mingine inayofanya kazi duniani kote, shirika hilo limesema.

Mapanga ya mtambo huo yana urefu wa mita 123 kila moja na yanaweza kuzunguka kuvuta upepo kwenye eneo lenye ukubwa wa takriban mita za mraba 50,000 -- kiasi ambacho ni sawa na ukubwa wa viwanja saba vya kawaida vya soka.

Inakadiriwa kuwa mtambo huo utaaweza kuzalisha umeme wenye uwezo wa zaidi ya kilowati milioni 66 kwa saa kila mwaka, kukidhi mahitaji ya kila mwaka ya matumizi ya umeme ya kaya 36,000 zenye watu watatu. Hiyo ni sawa na kuokoa takriban tani 22,000 za makaa ya mawe na kupunguza utoaji wa hewa kaboni kwa takriban tani 54,000.

Lei Mingshan, Mwenyekiti wa Shirika la China Three Gorges, amesema mtambo huo ni mafanikio katika teknolojia ya msingi ya mnyororo wa viwanda vya nishati ya upepo baharini, na utakuza maendeleo endelevu ya tasnia ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha