

Lugha Nyingine
Hejian: Mji unaojulikana kwa uzalishaji wa glasi kaskazini mwa China (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2023
![]() |
Mfanyakazi akichonga bidhaa kwenye karakana ya glasi huko Hejian, katika Mji wa Cangzhou, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China. (Picha kwa hisani ya Kampuni ya Teknolojia ya Vioo ya Hebei Mingshangde) |
Hejian, mji ulioko mji wa Cangzhou, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, ndiyo kitovu kikubwa zaidi cha uzalishaji wa glasi inayostahimili joto.
Mji huo unajivunia kuwa na zaidi ya kampuni 200 za glasi, zikiajiri zaidi ya watu 60,000. Bidhaa za glasi kutoka mji huo zimechukua nafasi kubwa siyo tu katika soko la ndani ya China lakini pia kimataifa, na husafirishwa kwa zaidi ya nchi na maeneo 50. Mwaka 2022, pato la Hejian lilifikia karibu yuan bilioni 10 (dola bilioni 1.38 za Kimarekani), na kuwa nguzo kubwa ya utulivu na maendeleo ya biashara ya nje ya Cangzhou.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma