Kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na tembo mkoani Yunnan, Kusini Magharibi mwa China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2023
Kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na tembo mkoani Yunnan, Kusini Magharibi mwa China
Tembo wa Asia wakionekana katika Wilaya inayojiendesha ya Makabila ya Wahani na Wayi ya Jiangcheng iliyoko Pu'er, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, Julai 19, 2023. (Xinhua/Fei Maohua)

Tembo wa Asia, spishi kuu katika mfumo ikolojia wa misitu ya mvua, wako chini ya uhifadhi wa kitaifa wa daraja la kwanza nchini China. Wengi wa Tembo hao hupatikana Yunnan.

Mwaka 2011, tembo 18 wa Asia walifika kwenye Wilaya hiyo ya Jiangcheng. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, zaidi ya tembo 20 wamezaliwa hapa.

Serikali ya mtaa imewawekea bima wakulima ili kulinda mali zao, na kuunda timu ya kuchunguza na kufuatilia tembo hao usiku na mchana ili kuhakikisha usalama wa wanakijiji wanapoishi kwa pamoja na tembo hao.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha