Bustani ya wazi ya mabaki ya kihistoria yafungua eneo jipya kwa ajili ya umma huko Chengdu, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2023
Bustani ya wazi ya mabaki ya kihistoria yafungua eneo jipya kwa ajili ya umma huko Chengdu, China
Picha hii iliyopigwa kutoka angani Julai 20, 2023 ikionyesha bustani ya nje ya makazi ambayo ni mabaki ya kihistoria huko Chengdu, Mji Mkuu wa Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Shen Bohan)

Bustani hiyo ya mabaki ya kihistoria imefungua eneo jipya kwa ajili ya umma siku ya Alhamisi huko Chengdu. Bustani hiyo iko katikati ya eneo la mji wa kale wa Chengdu. Tangu Mwaka 2013, wanaakiolojia wa China wamegundua sehemu kubwa yenye mabaki ya mji wa kale kutoka Mtaa wa Donghuamen hadi Kituo cha Michezo cha Chengdu katika Eneo la Qingyang la mji wa Chengdu, ukubwa wa sehemu iliyofukuliwa ilifikia mita za mraba 49,000, hasa ikihusisha mabaki ya Kipindi cha Mapigano ya Madola (475-221 KK), Enzi ya Qin (221-207 BC) na Enzi ya Han (202 BC-220 AD), Enzi za Sui na Tang (581-907), Enzi ya Song (960-1279) na Enzi ya Ming (1368-1644). (Xinhua/Shen Bohan) 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha