

Lugha Nyingine
China yarusha satelaiti nne kwenye anga ya juu (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2023
TAIYUAN - China imerusha roketi ya Long March-2D kwenye anga ya juu, na kutuma satelaiti 4 kwenye obiti iliyopangwa mapema.
Roketi hiyo iliondoka saa 4:50 asubuhi (Saa za Beijing) kutoka Kituo cha Kurusha Satelaiti kwenye anga ya juu cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China siku ya Jumapili.
Satelaiti tatu kati ya hizo zitatumika kupata data za uchunguzi wa kuhisi kutoka mbali na kutoa huduma za kibiashara za kuhisi kwa mbali, huku satelaiti nyingine itatumika kwa uthibitishaji wa teknolojia ya mawasiliano ya satelaiti.
Hii ni safari ya 479 kwenye anga ya juu kwa kizazi cha roketi za Long March.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma