“Ateri za Kijani” kwenye Jangwa la Kubuqi la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 25, 2023
“Ateri za Kijani” kwenye Jangwa la Kubuqi la China
Picha iliyopigwa tarehe 21, Julai ikionesha barabara ya kwanza ya kupitia jangwani kwenye Wilaya ya Hangjin iliyojengwa mwaka 1999 (Picha imepigwa kwa droni). Picha na Liu Lei/Mwandishi wa Habari wa Xinhua.

Wakati wa majira ya joto, barabara kuu za zinapitia Jangwa la Kubuqi katika Wilaya ya Hangjin, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani nchini China, na mimea ya kijani imestawi kikamilifu pembezoni mwao, kama “ateri za kijani” kwenye jangwa hilo.

Tangu barabara ya kwanza ya kupitia jangwani huko ilipokamilishwa mwaka 1999, urefu wa jumla wa barabara za kupitia jangwani katika Wilaya ya Hangjin umefikia kilomita 930. Barabara hizo za kupitia jangwani siyo tu zimeleta urahisi kwa wakazi huko waliokuwa wamezuiliwa na jangwa siku za nyuma na hawakuwa na namna ya usafiri, bali pia zimeweka msingi imara kwa utekelezaji miradi ya kuzuia na kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa na uwekezaji wa kampuni kwenye jangwa la Kubuqi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha