Kundi la 13 la China la Utafiti wa Kisayansi wa Bahari ya Aktiki lavuka Mzingo Aktiki (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2023
Kundi la 13 la China la Utafiti wa Kisayansi wa Bahari ya Aktiki lavuka Mzingo Aktiki
Picha iliyopigwa tarehe 25, Julai kutoka meli ya “Xuelong 2” ikionesha barafu inayoelea ndani ya Mzingo wa Aktiki.

Kwa mujibu wa utangazaji kwenye meli ya “Xuelong 2”, ambayo ni meli ya utafiti wa kisayansi ya kuvunja barafu kwenye eneo la ncha, Kundi la 13 la China la utafiti wa kisayansi wa Bahari ya Aktiki limevuka Mzingo wa Aktiki tarehe 24, Julai saa 10 na dakika 34 Jioni (kwa saa za Beijing) na kuingia kwenye maji ya Bahari ya Aktiki na kuendelea safari yake ya kitafiti.

Tarehe 12, Julai, kundi hilo lilipanda meli hiyo ya “Xuelong 2” kuondoka Shanghai na kuelekea Bahari ya Aktiki kutekeleza kazi za utafiti wa kisayansi. Katika siku 12 zilizopita, meli ya “Xuelong 2” ilipita Bahari ya Mashariki ya China, Bahari ya Japan, Bahari ya Okhotsk, na Bahari ya Bering, ikaelekea Kaskazini kupita Mlango-Bahari wa Bering na kufikia Mzingo wa Aktiki kwa mafanikio.

Baada ya kuingia kwenye Mzingo wa Aktiki, kundi hilo la utafiti litaendelea kwenda kwenye sehemu ya kazi iliyopangwa. Ratiba inaonesha kuwa, meli “Xuelong 2” inatarajiwa kufika kwenye Mkondo wa Chukchi tarehe 26, ambapo kundi hilo litaanza rasmi utafiki wa kisayansi wa Bahari ya Aktiki.

Picha zimepigwa na Wei Hongyi/Mwandishi wa Habari wa Xinhua

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha