Rais Xi Jinping akagua Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2023
Rais Xi Jinping akagua Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China
Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akitembelea sehemu moja ya mabaki ya mfumo wa njia ya kale inayojulikana kwa jina la "Shudao" katika Mji wa Guangyuan, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, Julai. 25, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

CHENGDU - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amekagua Mkoa wa Sichuan ulioko Kusini Magharibi mwa China siku ya Jumanne na Jumatano.

Ametembelea sehemu moja ya mabaki ya mfumo wa njia ya kale inayojulikana kwa jina la "Shudao" katika Mji wa Guangyuan na Jumba la Makumbusho la Sanxingdui katika Mji wa Deyang, mtawalia.

Rais Xi amefahamishwa juhudi zinazofanywa za kuhimiza urithishaji wa kihistoria na kiutamaduni na uhifadhi wa ikolojia, maendeleo katika ufukuaji na utafiti wa mabaki ya kale ya kihistoria na kiutamaduni, pamoja na uhifadhi na urejeshaji wa mabaki ya kitamaduni. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha