"Uchumi wa maua" wasaidia ustawishaji wa vijijini huko Qianxi, Mkoa wa Guizhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2023

Mnamo Julai 24, maua yaliyopandwa katika Kijiji cha Qianhua kilichoko Kitongoji cha Guli katika Mji wa Qianxi, Mkoa wa Guizhou, Kusini Magharibi mwa China yaliingia katika kipindi cha kuchanua. Wakulima wamenza kuchuma maua hayo na kuyapeleka sokoni.

Katika miaka ya hivi karibuni, kitongoji hicho cha Guli kimelenga mahitaji ya soko la maua, kutekeleza mfumo wa "ushirika + kampuni + wakulima", kurekebisha kikamilifu muundo wa seketa ya kilimo na kuongoza wakulima wenyeji kuendeleza upandaji wa maua ya kipekee, kama vile gerbera, alizeti, krisanthemum n.k. ili kuongeza mapato ya wakulima na kuchangia ustawishaji wa vijijini. (Picha na Zhou Xunchao/Tovuti ya Gazeti la Umma)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha