Mbio za Kukimbiza Mwenge wa Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Chengdu zafikia mwisho (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2023
Mbio za Kukimbiza Mwenge wa Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Chengdu zafikia mwisho
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Tarehe 26, Julai, mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani (FISU) ya majira ya joto ya Chengdu zilikamilika. Siku hiyo mwenge ulikimbizwa kwenye Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Kusini Magharibi (Kampasi ya Jiuli), Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Chengdu, Chuo Kikuu cha Chengdu na sehemu kuu itakayotumika kwa michezo hiyo, Eneo Maalum la kumbi za Michezo la Ziwa Dong'an katika Mji wa Chengdu, China, ikiashiria mwisho wa mbio za kukimbiza mwenge huo kwa kupokezana zilizodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Moto wa mwenge wa michezo ya FISU ya Chengdu ulichukuliwa katika Mji wa Turin wa Italia, ambako michezo ya kwanza ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani ya majira ya joto ilifanyika. Baada ya moto huo kufika Chengdu, uliunda mwenge unaoitwa “Moto wa Chengdu” ambao umekimbizwa kwa siku 49 kwenye miji ya Beijing, Harbin, Shenzhen, Chongqing, Yibin na Chengdu ya China, ukipitia vyuo vikuu 25 nchini humo. Wabeba mwenge zaidi ya 800 wameshiriki kwenye mbio hizo za kupokezana mwenge.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha