China yapandisha mwitikio kwa ngazi ya juu dhidi ya Kimbunga Doksuri kinachozidi kuwa na nguvu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2023
China yapandisha mwitikio kwa ngazi ya juu dhidi ya Kimbunga Doksuri kinachozidi kuwa na nguvu
Picha hii ikionyesha boti za wavuvi zikiwa zimeegeshwa kwa ajili ya usalama bandarini wakati Kimbunga Doksuri kinapokaribia katika Mji wa Chaozhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Julai 27, 2023. (Picha na Yao Feng/Xinhua)

BEIJING – Idara ya Hali ya Hewa ya China imepandisha mwitikio wake dhidi ya kimbunga hadi ngazi ya kwanza, ambayo ni ya juu kabisa katika mwitikio wa tahadhari siku ya Alhamisi alasiri, kwani Kimbunga Doksuri kinabadilika kuwa kimbunga kikubwa cha kupita kiasi.

Kimbunga Doksuri, ambacho ni cha tano mwaka huu kuikumba China, kimeimarika kutoka kimbunga chenye kasi ndogo hadi kuwa chenye kasi kali siku ya Alhamisi alasiri na kilishuhudiwa umbali wa takriban kilomita 360 Kusini Mashariki mwa Mji wa Xiamen katika Mkoa wa Fujian nchini China saa 11 jioni.

Taarifa iliyotolewa na serikali imesema kuwa, kimbunga hicho kitahamia kaskazini-magharibi kwa kasi ya kilomita 15 hadi 20 kwa saa huku kikizidi kuwa na nguvu zaidi.

“Kimbunga Doksuri kinatazamiwa kufika katika maeneo ya pwani kati ya miji ya Dongshan na Putian katika Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China siku ya Ijumaa asubuhi,” taarifa hiyo imesema.

Serikali imezitaka mamlaka husika za hali ya hewa katika mikoa ya Fujian, Guangdong, Zhejiang na Jiangxi, kupandisha ngazi za mwitikio cha kukabiliana na hali ya dharura kulingana na hali za maeneo husika, kuratibu kwa pamoja na idara za serikali zinazohusika, na kuongoza umma kuzuia majanga na kuepuka hatari.

Kituo cha kitaifa cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha China Alhamisi asubuhi kilitoa tahadhari nyekundu kwa Kimbunga Doksuri, ambayo ni tahadhari ya juu zaidi katika mfumo wake wa tahadhari wenye ngazi nne, kwani kimekadiria kuwa, kimbunga hicho kitaleta upepo mkubwa na mvua kubwa katika maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha