

Lugha Nyingine
Mkutano wa Pili wa Viongozi Wakuu wa Russia na Afrika waanza St. Petersburg, Russia (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2023
![]() |
Mshiriki akitembelea maonyesho kwenye Mkutano wa pili wa Viongozi Wakuu wa Russia na Afrika huko St. Petersburg, Russia, Julai 27, 2023. (Picha na An Xiaomeng/Xinhua) |
ST. PETERSBURG - Mkutano wa pili wa viongozi wakuu wa Russia na Afrika umeanza Alhamisi katika Mji wa St. Petersburg, nchini Russia.
Kwenye mkutano huo utakaofanyika kwa siku mbili, viongozi watajadili fursa za ushirikiano katika chakula, nishati, nafasi ya anga, teknolojia ya habari, elimu na michezo.
Msaidizi wa Ikulu ya Russia, Kremlin Yuri Ushakov alisema Jumanne kuwa nchi 49 za Afrika zitatuma wawakilishi na wajumbe kwenye mkutano huo, na wakuu wa nchi 17 na baadhi ya wakuu wa mashirika makubwa ya kikanda ya Afrika watashiriki.
Mkutano wa kwanza wa viongozi wakuu wa Russia na Afrika ulifanyika katika mji wa mapumziko wa Russia ulioko Bahari Nyeusi wa Sochi Oktoba 2019.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma