Habari ya picha: Mhandisi wa Umeme kutoka Kenya aliyehitimu masomo yake nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 01, 2023
Habari ya picha: Mhandisi wa Umeme kutoka Kenya aliyehitimu masomo yake nchini China
David Maina Kamore anakagua michoro kwenye kambi ya eneo la ujenzi wa kituo cha transfoma cha Konza katika Kaunti ya Machakos, Kenya, Juni 12, 2023. (Xinhua/Han Xu)

David Maina Kamore, 32, ni mhandisi wa umeme katika kituo cha transfoma cha Konza, taaluma ambayo anaipenda tangu akiwa mtoto.

Mwaka wa 2009 alikuja China ambako alipata mafunzo ya lugha ya Kichina kwa mwaka mmoja, katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Huazhong na baadaye kuendelea na masomo ya uhandisi wa umeme na mitambo katika Chuo Kikuu cha Chang'an.

Mwaka 2014 baada ya kuhitimu masomo ya shahada ya kwanza ya uhandisi, David aliamua kutumia elimu yake kwa kufanya mazoezi katika mji wake, na tangu wakati huo alipata uzoefu mkubwa.

Mwaka 2022, katika hatua muhimu ya ujenzi wa kituo cha transfoma cha Konza, David alituma maombi ya kazi kwa Kampuni ya China Aerospace Construction Group (CACGC), iliyokuwa inatekeleza kandarasi ya ujenzi wa kituo kidogo cha 400kV. Hii pia ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kufanya kazi na umeme wa gridi kuu.

Kituo hicho kidogo kilicho umbali wa kilomita 70 kusini mashariki mwa Nairobi, ni sehemu ya Mradi wa Upanuzi wa Usambazaji Umeme nchini (KPTEP), mradi muhimu ulio chini ya Mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia moja”. Pia ni kituo cha ziada cha eneo la teknolojia la Konza, moja ya miradi muhimu ya mpango wa maendeleo wa Kenya kuelekea mwaka 2030 (Vision 2030).

"Naishukuru China kwa kunisaidia kutimiza ndoto yangu, na kushiriki kwenye ujenzi wa mji wangu ni jambo la furaha sana kwangu. Natarajia kuwa tunachokifanya kitawanufaisha watu wa Kenya," mhandisi huyo aliiambia mwandishi wa habari wa Xinhua.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha