Barabara za milimani zaleta urahisi na manufaa ya kiuchumi kwa wakazi wa Kusini mwa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2023
Barabara za milimani zaleta urahisi na manufaa ya kiuchumi kwa wakazi wa Kusini mwa China
Picha hii iliyopigwa kwa droni tarehe 31, Julai, ikionesha "Barabara ya Longguai" inayoelekea kitongoji cha Bainan kutoka kitongoji cha Gechoutun katika Wilaya ya Napo, Mkoa unaojiendea wa Guangxi, Kusini Magharibi mwa China. (Picha na Zhang Ailin/Xinhua)

Katika Mkoa wa Guangxi, ugumu wa kusafiri ulikuwa tatizo kubwa katika maisha ya watu wa vijijini katika sehemu kubwa ya milimani.

Katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uungaji mkono wa Chama na serikali, watu wa sehemu hiyo wamejenga barabara nyingi zinazozunguka milima yenye miteremko mikali inayoitwa na watu kuwa ni "Barabara ya Longguai", maana yake ya Kichina ni mikunjo ya dragoni. Barabara hizo sio tu zimetatua tatizo la "ugumu wa kusafiri" kwa wakazi wa huko, bali pia zimekuwa "njia ya haraka" ya kuongeza mapato na kupata ustawishaji wa vijiji kwa wanavijiji milimani.

Barabara inayoelekea kitongoji cha Bainan kutoka kitongoji cha Gechoutun huko Wilaya ya Napo, Mkoa unaojiendesha wa Guangxi ndiyo barabara yenye sura hii. Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Xinhua alipiga picha kwa droni mwonekano mzuri wa "Barabara ya Longguai".

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha