Siku ya Nne ya Michezo ya Chengdu Universiade: China yajiongezea medali 10 za dhahabu, na rekodi tatu za michezo hiyo zimevunjwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2023
Siku ya Nne ya Michezo ya Chengdu Universiade: China yajiongezea medali 10 za dhahabu, na rekodi tatu za michezo hiyo zimevunjwa
Mchezaji Wang Xiaotong wa China akipambana na Kuruno Aoi wa Japan kwenye fainali ya mchezo wa mpira wa meza kwa wanawake, kwenye Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia (FISU) inayoendelea mjini Chengdu, kusini-magharibi mwa Mkoa wa Sichuan. Agosti 1, 2023. (Xinhua/Zhao Zishuo)

China imejiongezea medali 10 zaidi za dhahabu kwenye orodha ya jumla ya medali zake za mkusanyiko wake kwenye michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia inayoendelea huko Chengdu, huku kuwa na rekodi tatu mpya za michezo hiyo wakati mashindano ya kuogelea yakianza Jumanne.

Ni hivi karibuni tu baada ya kushiriki kwenye Mashindano ya kuogelea ya dunia huko Fukuoka, Japan, mabingwa wa Olimpiki ya Tokyo, Zhang Yufei na Li Bingjie, waliiongoza Timu ya China kupata ushindi katika mashindano ya kuogelea kwa kupokezana mita 4x100 kwa wanawake, kwa kutumia dakika tatu na sekunde 37.51 na kuweka rekodi mpya ya michezo hiyo.

Muda mfupi baada ya Gallagher Erin Paige wa Afrika Kusini kuvunja rekodi ya mchezo wa kuogelea mita 50 kwa mtindo wa kipepeo kwenye nusu fainali, Zhang aliogelea haraka zaidi kwa sekunde 0.43.

Wakati huo huo, bingwa wa dunia Qin Haiyang wa China pia alivunja rekodi ya michezo hiyo katika nusu fainali ya mita 100 kwa wanaume, na kufanikiwa kuingia fainali pamoja na mwenzake Song Jiale.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha