Mtoto mchanga wa panda afikia umri wa mwezi mmoja katika Bustani ya Wanyama ya Chongqing (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2023
Mtoto mchanga wa panda afikia umri wa mwezi mmoja katika Bustani ya Wanyama ya Chongqing
Picha hii iliyopigwa Agosti 5 ikionesha mtoto mchanga wa panda. (Picha inatolewa na Bustani ya Wanyama ya Chongqing)

Habari kutoka Bustani ya Wanyama ya Chongqing zimesema, panda "Mangzai" alizaa mtoto wa kiume saa 14:12 mchana tarehe 6, Julai. Hii ni mara ya tatu kwa panda "Mangzai" kuzaa watoto.

Mtoto huyo mchanga wa panda amefikia umri wa mwezi mmoja tarehe 6, Agosti, na Bustani ya Wanyama ya Chongqing ilitangaza hali ya kuzaliwa kwake kwa mara ya kwanza. Mnamo mwezi Machi mwaka huu, panda "Mangzai" alikutana na panda "Jinke" katika Kituo cha Uhifadhi na Utafiti cha Panda cha China. Julai 6 mwaka huu, panda "Mangzai" alizaa mtoto wa panda mwenye uzito wa gramu 191, ambaye ni panda mchanga mzito zaidi aliyezaliwa katika Bustani ya Wanyama ya Chongqing. Sasa uzito wa mtoto huyu mchanga wa panda umefikia gramu 1439.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha