

Lugha Nyingine
Idadi ya Kulungu nchini China yaongezeka kutokana na juhudi za uhifadhi (2)
![]() |
Picha hii iliyopigwa kutoka angani Agosti 1, inaonesha Kulungu dume aina ya Milu (Kwenye kona juu kulia) akifukuzia majike katika hifadhi ya taifa ya Shishou, Mkoani Hubei, China. (Xinhua/Wu Zhizun) |
Kulungu aina ya Milu walio kwenye hifadhi ya taifa ya Shishou, huwa wanazaliana kati ya mwezi Juni na Agosti kila mwaka, wakati ambapo madume hupambana kutafuta fursa ya kuwa na majike wengi kadri iwezekanavyo. Ili kuhakikisha mazingira salama na tulivu kwa ajili ya kuzaliana kwao, walinzi wa wanyamapori kwenye hifadhi hii wamekuwa wakitumia muda mwingi na kufanya juhudi kubwa zaidi kufanya doria.
Baada ya juhudi za miaka mingi za walinzi wa mazingira na uboreshaji unaoendelea wa mazingira ya asili kwenye hifadhi hiyo, idadi ya Kulungu kwenye hifadhi hii imeongezeka kwa kasi, na sasa inakaribia kufika 2,000. Kuna zaidi ya vikundi 10 vya ufugaji wa asili vilivyoundwa kwa ukubwa tofauti kati ya Kulungu hawa wa Milu, na kulungu wengi zaidi wa aina hiyo wanatarajiwa kuzaliwa baada ya msimu wa kupandana mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma