

Lugha Nyingine
Wanakijiji wachuma uyoga wa porini milimani huko Yunnan, Kusini Magharibi mwa China (5)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2023
Wakati msimu wa mvua inapokuja, uyoga wa porini unachipuka katika milima huko Wilaya ya Nanhua, Mji unaojiendesha wa Kabila la Wayi wa Chuxiong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China. Wanakijiji wenyeji wanashughulikia kuchuma uyoga.
Nanhua iko katikati ya Mkoa wa Yunnan. Wilaya hiyo ina aina mbalimbali za misitu na maeneo makubwa ya misitu, pia ina maliasili nyingi za uyoga wa porini. Hadi sasa, zaidi ya aina 290 za uyoga wa porini unaoweza kuliwa zimegunduliwa katika wilaya hiyo, na zaidi ya tani 10,000 za uyoga wa porini unaoweza kuliwa zinatengenezwa huko kila mwaka.
Mwaka jana, tani 11,100 za uyoga wa porini ziliuzwa huko Nanhua, ambazo zina thamani ya Yuani bilioni 1.32 (sawa na dola za kimarekani milioni 184.5).
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma