

Lugha Nyingine
Mkutano wa Maendeleo ya Shughuli za Utunzaji wa Afya kufanyika tarehe 24 Jincheng, China (3)
Tarehe 10, Agosti, kwenye mkutano wa utoaji wa habari kuhusu Mkutano wa Shanxi (Jincheng), China 2023 wa Maendeleo ya Shughuli za Utunzaji wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi No.1 wa Tovuti ya Gazeti la Umma hapa Beijing, mjumbe wa kudumu wa kamati ya Chama cha CPC ya Mji wa Jincheng Wu Jianpeng, ambaye pia ni naibu meya na mkuu wa uenezi wa mji huo alialika kwa udhati watu wa China na nchi nyingine duniani waje Jincheng kushuhudia hali ya maendeleo ya shughuli za utunzaji wa afya kuanzia tarehe 25 hadi 27 mwezi huu.
Mjumbe wa kamati ya chama cha CPC ya Tovuti ya Gazeti la Umma Pan Jian, ambaye pia ni mkurugenzi wa bodi na naibu meneja mkuu wa tovuti hiyo, mjumbe wa kikundi cha uongozi wa CPC cha Idara ya utamaduni na utalii ya Mkoa wa Shanxi Chen Shaoqing, ambaye pia ni naidu mkuu wa idara hiyo na viongozi wengine walihudhuria kwenye mkutano huo wa utoaji habari.
Habari zinasema kuwa mkutano huo una kaulimbiu ya “maendeleo ya shughuli za utunzaji afya yaonekana eneo zima”. Ukumbi mkuu wa mkutano utakuwa kwenye eneo la vielelezo vya utunzaji wa afya wa ngazi ya juu la Mlima Baimasi katika Mji wa Jincheng, na wakati wa mkutano kufanyika, kutakuwa na shughuli mbalimbali, zikiwemo tamasha la utalii kwa ajili ya utunzaji wa afya, shughuli ya kuvutia uwekezaji katika shughuli za utunzaji wa afya n.k.
Mji wa Jincheng uko kwenye Kusini-Mashariki mwa Mkoa wa Shanxi wa China, ukiwa ni “Mji wa kwanza wa vielelezo vya shughuli za utunzaji wa afya Duniani” nchini China, na mji mwenyeji wa kudumu wa kuitisha Mkutano wa Maendeleo ya Shughuli za Utunzaji wa Afya. Hadi sasa mkutano huo umefanyika kwa mafanikio kwa miaka mitatu mfululizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma