Daraja la Mto Changjiang la Nanjing lafungwa kingo cha kuzuia meli zisigonge nguzo za daraja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 11, 2023
Daraja la Mto Changjiang la Nanjing lafungwa kingo cha kuzuia meli zisigonge nguzo za daraja
Wafanyakazi wa Shirika la Reli la China Tawi la Shanghai wakifunga kingo cha kuzuia meli zisigonge nguzo za daraja kwenye Daraja la Mto Changjiang la Nanjing huko Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Agosti 9. (Picha ilipigwa kwa droni.)

Nguzo za namba ya 3, 4 na 5 za Daraja la Mto Changjiang la Nanjing zilifungwa bila matatizo kingo cha kuzuia meli zisigonge nguzo na kuanza kutumika Agosti 10. Habari zinasema kwamba kwa kulingana na umaalumu wa eneo la Mto Changjiang na hali yake ya usafirishaji, kingo cha kuzuia meli zisigonge nguzo za daraja kilichofungwa wakati huo kinaweza kuelea juu na chini kufuatana na kiwango cha maji. Pia, kingo hicho kinaweza kupokea, kutawanya au kuhamisha kwa ufanisi nguvu zilizotokana na meli ilipogongana na kingo, ili kuepusha kupinduka na kuzama kwa meli.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha