“Ghuba kwa wafanyakazi” yawawezesha wanaofanya kazi nje ya nyumba kupumzika kwa starehe  huko Chongqing (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 14, 2023
“Ghuba kwa wafanyakazi” yawawezesha wanaofanya kazi nje ya nyumba kupumzika kwa starehe  huko Chongqing
Agosti 12, wasafishaji kadhaa wakiingia kwenye “ghuba kwa wafanyakazi” na kupumzika katika Mtaa wa Zhuangzhi wa Eneo la Shapingba la Mji wa Chongqing.

Katika siku hizi mfululizo, Mji wa Chongqing umeendelea kukumbwa na joto kali sana. "Ghuba kwa wafanyakazi" iliyoanzishwa katika Eneo la Shapingba la Mji wa Chongqing imekuwa mahali pa kupumzika na kuepusha joto kwa wafanyakazi wengi wanaofanya kazi nje ya nyumba.

“Ghuba kwa wafanyakazi” ni mahali pa kutoa huduma kwa wanaofanya kazi nje ya nyumba kama vile wasafishaji, wafanyakazi wa bustani, wapeleka vifurushi, na maafisa wa idara ya usimamizi wa miji, ili waweze kupumzika kwa muda katika wakati wa kazi, ambapo wasafishaji wanaweza kupata kifungua kinywa kwa bure, kutumia mashine za microwave, jokofu, vyumba vya kupumzika n.k., na mahali hapo pia panatoa maji bure ya kunywa kwa wakazi wa mjini, kutoa mashauriano, kuwawezesha watu kupata charge ya simu za mkononi, huduma ya matibabu ya dharura na huduma nyingine zinazowasaidia watu.

Habari zinasema kuwa, hadi sasa mji wa Chongqing umejenga na kufungua sehemu1320 za “ghuba kwa wafanyakazi”. (Picha na Huangwei/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha