

Lugha Nyingine
Viongozi wa Misri, Jordan na Palestina wahimiza kukomesha uvamizi wa Israel na kurejesha mazungumzo ya amani
CAIRO - Viongozi wa Misri, Jordan na Palestina wamesisitiza ulazima wa kukomesha uvamizi wa Israel katika ardhi ya Palestina ili kurejesha amani na mambo ya Palestina, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Misri siku ya Jumatatu.
Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri, Mfalme Abdullah II wa Jordan, na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wamefanya mkutano wa pande tatu katika mji wa pwani ya Misri wa New Alamein, ambapo viongozi hao watatu wamesisitiza maendeleo mapya ya mambo ya Palestina.
Viongozi hao wamesisitiza haja ya wananchi wa Palestina kupata haki zao zote halali, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa nchi huru na inayojitawala juu ya msingi wa mipaka iliyothibitishwa Mwaka 1967 huku Jerusalem Mashariki ukiwa mji mkuu wake, kutatua suala la wakimbizi wa Palestina kwa mujibu wa azimio halali la kimataifa, na kupata suluhisho la nchi mbili kwa mujibu wa marejeleo yaliyoidhinishwa.
Viongozi hao pia wamesisitiza ulazima wa Israel kutekeleza wajibu na ahadi zake kwa mujibu wa sheria za kimataifa, sheria za kimataifa za kibinadamu, mikataba na maelewano ya awali ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na matokeo ya mkutano wa al-Aqaba.
Viongozi hao wameitaka Israel isitishe mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina na uvamizi katika maeneo yanayokaliwa kimabavu na walowezi wa Israel ya Ukingo wa Magharibi, na kuitaka Israel iondoe vikwazo kwenye Ukanda wa Gaza.
Zaidi ya hayo, viongozi hao wameitaka Israel iachilie fedha za Palestina inazozishikilia bila msingi wowote wa kisheria.
Viongozi hao watatu wameelezea nia yao ya kuendeleza juhudi zao na wahusika wakuu wa kimataifa na kufufua mchakato makini wa amani kwa misingi ya sheria za kimataifa, marejeo ya amani, ndani ya utaratibu, na ratiba maalum.
Misri, ambayo ilitia saini mkataba wa amani na Israel Mwaka 1979, imesisitiza mara kwa mara msimamo wake unaounga mkono kuanzishwa kwa nchi huru ya Palestina kwa kuzingatia suluhu ya kuundwa kwa nchi mbili inayotambuliwa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma