Timu ya madaktari wa China yatoa ujuzi wa Dawa za Mitishamba za Kichina kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2023
Timu ya madaktari wa China yatoa ujuzi wa Dawa za Mitishamba za Kichina kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Namibia
Wanafunzi wakifanya mazoezi ya kupigana kwa mitindo nane ya viungo yanayojulikana kwa jina la Baduanjin Qigong kwenye mhadhara wa dawa za mitishamba za Kichina (TCM) katika Chuo Kikuu cha Namibia huko Windhoek, Namibia, Agosti 14, 2023. (Xinhua/Chen Cheng)

WINDHOEK - Timu ya madaktari wa China nchini Namibia imetoa mhadhara kuhusu dawa za mitishamba za Kichina (TCM) kwa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Namibia, na kuwawezesha kuelewa vyema mbinu za dawa hizo.

Kwenye mhadhara uliofanyika Jumatatu katika Taasisi ya Confucius ya chuo kikuu hicho, madaktari hao wa China wametoa maelezo ya kina kuhusu dawa hizo, katika hatua iliyokusudiwa kuwafahamisha na kuwaelimisha wanafunzi zaidi juu ya faida za dawa za mitishamba za Kichina kama njia mbadala ya matibabu mengine ya kisasa.

Timu hiyo ya madaktari wa China imeelezea matumizi ya mbinu za matibabu kama vile acupuncture na namna na kwa nini yanatolewa, na jinsi mbinu nyingine zinavyounganishwa ili kuwa na ufanisi zaidi, kama vile kutumia tiba ya moxibustion kwa pamoja na acupuncture kama njia ya asili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali.

Madaktari hao pia wamesisitiza faida za dawa za mitishamba za Kichina, wakisema zinachukuliwa kuwa zisizo za maumivu na hazina athari kali kama dawa nyingine.

Kwenye mhadhara huo, wanafunzi walipata fursa ya kupata uzoefu wa baadhi ya mbinu za tiba za kijadi za China ikiwa ni pamoja na acupuncture, masaji, moxibustion, na kikombe.

Kaputuaza Mbuende, mwanafunzi wa mwaka wa pili, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa uzoefu wote ulikuwa wa kuvutia. "Huu ulikuwa uzoefu wangu wa kwanza kupata tiba ya acupuncture na nimejifunza mengi kutoka kwa historia ya mbinu huo," amesema.

Kwa mujibu wa Mbuende, miezi kadhaa iliyopita alivunjika mkono na tangu wakati huo imekuwa vigumu kusogeza baadhi ya vidole vyake kutokana na kuathirika kwa mishipa kulikosababishwa na jeraha lake.

China hadi sasa imetuma jumla ya timu 15 za madaktari nchini Namibia tangu ujumbe wake wa kwanza Mwaka 1996. Timu za madaktari zimejitolea kuhakikisha afya ya watu wa Namibia huku pia zikidumisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha