Habari Picha ya walinzi wa Hoh Xil, eneo la makazi muhimu kwa swala wa Tibet huko Qinghai wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2023
Habari Picha ya walinzi wa Hoh Xil, eneo la makazi muhimu kwa swala wa Tibet huko Qinghai wa China
Wafanyakazi wa kituo cha ulinzi cha Ziwa Drolkar cha ofisi ya usimamizi ya Hoh Xil wakiwa katika picha ya pamoja huko Hoh Xil, Mkoa wa Qinghai, Kaskazini-Magharibi mwa China, Juni 16, 2023. Ikiwa iko katika Hifadhi ya Taifa ya Sanjiangyuan, Hoh Xil ni makazi muhimu kwa swala wa Tibet ambao ni hifadhi ya kitaifa ya daraja la kwanza nchini China. Karibia Mwezi Mei kila mwaka, makumi ya maelfu ya swala wajawazito wa Tibet huanza kuhamia Hoh Xil ili kujifungua, wakiondoka na watoto wao mwishoni mwa Julai. Eneo la Ziwa Drolkar huko Hoh Xil ni mahali pa kuzaliana kwa spishi hiyo. (Xinhua/Zhang Hongxiang)

Ikijulikana kuwa mojawapo ya uhamaji kwa makundi wa kushangaza zaidi duniani wa wanyama wenye kwato, safari hii ya swala wa Tibet lazima ikabiliane na hali mbaya ya hewa na uvamizi wa wanyama pori. Walinzi hawa wa Hoh Xil wamekuwa wakiwalinda swala wa Tibet kwa miongo kadhaa.

Hoh Xil inajulikana kama eneo kubwa zaidi la China la urithi wa asili wa Dunia, ikidumisha mfumo wa ikolojia wa mwinuko na spishi za kipekee za Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet. Tangu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Hoh Xil, vituo sita vya ulinzi vimeanzishwa kimoja baada ya kingine. Mbali na kufanya kazi kwa zamu, makundi ya wafanyakazi pia hufanya doria kwa pande zote ndani ya eneo la hifadhi mara kwa mara. Doria ndogo hufanyika mara moja kila baada ya siku tatu wakati doria kubwa hufanyika angalau mara moja kwa mwezi. Hadi sasa, watu wa vizazi vitatu vya wafanya doria wamekuwa wakilinda ardhi ya Hoh Xil, ambayo imekuwa eneo muhimu kwa ulinzi wa wanyamapori na ulinzi wa kiikolojia nchini China. Idadi ya swala wa Tibet katika Hoh Xil imeongezeka kutoka chini ya 20,000 miaka ya 1980 hadi zaidi ya 70,000 sasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha