

Lugha Nyingine
Mpira wa wavu waamsha shauku ya hivi karibuni ya michezo vijijini kwenye kisiwa cha kitropiki cha Hainan, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2023
![]() |
Watu wakitazama mechi ya mpira wa wavu ya kijiji huko Wenchang, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Agosti 13, 2023.(Xinhua/Pu Xiaoxu) |
Ligi ya mpira wa wavu ya Hainan Wenchang Mwaka 2023, ambayo pia inajulikana kama mpira wa wavu wa kijijini, imekamilika huko Wenchang katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China hivi majuzi. Ligi hiyo iliyochukua mwezi mzima imeshirikisha timu 20 za wanaume kutoka Wenchang, Haikou, Qionghai na Chengmai. Wachezaji wengi ni wavuvi, wakulima na wachuuzi.
Ligi hiyo imevutia jumla ya watazamaji 485,800 na kuingiza mapato yenye thamani ya yuan milioni 280 yatokanayo na usafiri na utalii.
Kwa kuwa na historia ndefu katika mpira wa wavu, Wenchang inajivunia zaidi ya viwanja 600 vya mpira wa wavu na imeshuhudia mchezo huo ukipanda kwa umaarufu miongoni mwa wakazi wake.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma