Mkulima wa China aendesha hoteli kijijini karibu na daraja la juu zaidi duniani (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 21, 2023
Mkulima wa China aendesha hoteli kijijini karibu na daraja la juu zaidi duniani
Picha hii iliyopigwa Agosti 15, 2023 ikionyesha Daraja la Beipanjiang kwenye Barabara Kuu ya Hangzhou-Ruili, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Tao Liang)

Likiwa katika urefu wa zaidi ya mita 565.4 juu ya bonde, Daraja la Beipanjiang limetambulishwa kuwa daraja lenye urefu wa kwenda juu zaidi duniani na Shirika la Rekodi za Dunia la Guinness.

Katika miaka ya hivi majuzi, daraja hilo limekuwa kivutio maarufu kinachokaribishwa sana na watalii kwa sababu ya mandhari nzuri ya pembezoni mwake.

Ma Xuanjun, mkulima anayeishi karibu na daraja hilo alikarabati nyumba yake mpya ya matofali kuwa hoteli ya kijijini Mwaka 2019 na kuanza kupokea watalii kutoka mbali.

“Kabla ya kujengwa kwa daraja hilo, ilituchukua saa nne kupanda mlima hadi kwenye mji,” amesema Ma.

Sasa, hoteli yake kijijini imepambwa kwa picha alizopiga na watalii kutoka ndani na nje ya China.

"Watalii wengi hutembelea kijiji chetu kwa ajili ya daraja. Nitafanya kila niwezalo kuwafanya wajisikie furaha na kukumbuka maskani yangu ," Ma amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha