Handaki la ngao la barabara kuu ambalo ni refu zaidi nchini China lakamilika kuchimbwa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2023
Handaki la ngao la barabara kuu ambalo ni refu zaidi nchini China lakamilika kuchimbwa
Picha hii iliyopigwa Agosti 21, 2023 ikionyesha mashine ya kuchimba handaki la ngao katika kituo cha mradi wa handaki la ngao refu zaidi la barabara ya mwendo kasi mjini Beijing, China. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING – China imechimba handaki hapa Beijing Jumatatu kwa ajili ya usafiri wa barabara ya mwendo kasi. Hili ni handaki refu zaidi la barabara ya mwendo kasi nchini China lililochimbwa kwa kutumia mashine ya ngao.

Kampuni ya Kundi la Ujenzi wa Barabara kuu la Beijing inayotekeleza mradi huo imesema, handaki hilo likiwa na jumla ya urefu wa kilomita 7.4, limesanifiwa kuwa na barabara mbili zinazopishana zenye njia sita za kupitisha magari kwenye ngazi ya kati, njia ya moshi kwenye ngazi ya juu na njia za uokoaji na utoaji msaada wakati wa ajali katika ngazi ya chini.

Handaki hilo ni sehemu ya mradi wa barabara ya sita ya Mashariki ya mzunguko ya Beijing. Sehemu ya kina kabisa ya handaki hilo, ambayo iko umbali wa mita 75 kutoka juu hadi chini ya ardhi, ni handaki lililo chini kabisa mwa ardhi mjini Beijing kuliko mengine yote. Mwezi Juni, handaki la Magharibi la mradi huo lilikuwa la kwanza kuchimbwa. Handaki hilo la upande wa mashariki limechimbwa na kutobolewa tu siku ya Jumatatu.

Likiwa na kipenyo cha kuchimba cha mita 16.07 na urefu wa karibu mita 145, mashine hiyo ya kuchimba ya ngao iliyotumiwa katika mradi huo imeundwa na kukamilishwa kwa kujitegemea na kampuni za China. Ina uzito wa tani 4,500.

Mradi huo wa handaki umesaidia kutoa nafasi zaidi chini ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda na kupanga bustani kubwa, na kuchangia maendeleo yenye ubora wa juu ya Eneo la Tongzhou ambalo ni kiini cha pili cha utawala wa Beijing na kuratibu maendeleo ya usafiri katika sehemu za Beijing-Tianjin-Hebei.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha