Viongozi wa BRICS kujadili upanuzi wa wanachama huku nchi za Ulimwengu wa Kusini zikijipanga kujiunga (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2023
Viongozi wa BRICS kujadili upanuzi wa wanachama huku nchi za Ulimwengu wa Kusini zikijipanga kujiunga
Skrini za kielektroniki za mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS zikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 16, 2023. (Xinhua/Chen Cheng)

BEIJING - Nembo ya mkutano wa Mwaka 2023 wa wakuu wa ushirikiano wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) unaoanza leo ni jua yenye rangi tano: kijani, bluu, machungwa, nyekundu na njano, ikiwakilisha wanachama watano wa sasa wa ushirikiano huo.

Mkutano huo wa mwaka huu, utakaofanyika nchini Afrika Kusini kuanzia leo Agosti 22 hadi 24, unabeba kaulimbiu ya "Ushirikiano kwa Kuharakisha Ukuaji wa pamoja wa Uchumi, Maendeleo Endelevu na Ushirikiano jumuishi wa pande nyingi."

Maafisa wa BRICS wanasema, moyo huo umeibua shauku ya nchi zaidi ya 40 kutoka Ulimwengu wa nchi za Kusini kutaka kujiunga na ushirikiano huo.

Kuongezeka kwa shauku

Kwenye mkutano huu, viongozi wanatarajiwa kujadili upanuzi wa wanachama wa BRICS, ikiwa ni pamoja na vigezo vya kukaribisha wanachama wapya na kanuni elekezi, Carlos Maria Correa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusini, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

"Nchi nyingi za Ulimwengu wa nchi za Kusini zimejitahidi kushikamana ili kufanya kazi kwa pamoja kuelekea utaratibu wa Dunia wenye haki na jumuishi zaidi ... BRICS inahamasisha nchi nyingi kuungana tena ili kuendeleza maono haya," amesema Kenneth Creamer, mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, wakati wa mahojiano ya hivi karibuni na Xinhua.

Kwa mujibu wa habari, nchi takribani 40 zimeonyesha nia ya kujiunga na ushirikiano huo, zikiwemo, Algeria, Bangladesh, Misri, Falme za Kiarabu, Uruguay na nyingine nyingi.

Mvuto wa BRICS

Mwezi Juni mwaka huu, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwahi kueleza nia yake ya kuhudhuria mkutano huo kufuatia mazungumzo yake na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor.

Hapa ndipo haiba ya BRICS ilipo. Umoja huo umekuwa nguvu nzuri, imara na ya kiujenzi katika masuala ya kimataifa.

"Katika Dunia inayozidi kugawanika, BRICS inajenga mazingira wezeshi kwa nchi kuunda utaratibu jumuishi zaidi wa kisiasa na kiuchumi," amesema Cavince Adhere, msomi wa uhusiano wa kimataifa wa Kenya.

Matarajio mapana

Kukiwa na wanachama wapya wanaowezekana kujiunga, biashara ya kuvuka mpaka ndani ya BRICS itakuwa bora zaidi na kuvutia wawekezaji zaidi. Matarajio ya sarafu iliyotolewa na BRICS nayo yanawezekana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha