Rais Xi Jinping asisitiza juhudi kubwa zaidi za kujenga Xinjiang nzuri katika kutafuta Maendeleo ya Kisasa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2023
Rais Xi Jinping asisitiza juhudi kubwa zaidi za kujenga Xinjiang nzuri katika kutafuta Maendeleo ya Kisasa ya China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba wakati akifahamishwa kuhusu kazi ya kamati ya CPC na Serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, vilevile Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Xinjiang, huko Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Agosti 26, 2023. (Xinhua/Yan Yan)

URUMQI - Rais wa China Xi Jinping amehimiza kufahamu kwa uthabiti nafasi ya kimkakati ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang katika hali ya jumla ya kitaifa ya China na kujenga vema Xinjiang nzuri katika mchakato wa ujenzi wa kisasa ya China.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo siku ya Jumamosi alipopewa taarifa mjini Urumqi kuhusu kazi ya kamati ya CPC na Serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China, vilevile Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Xinjiang.

Ametaka kufanyika juhudi za pande zote, za uangalifu, thabiti na endelevu katika kuendeleza Xinjiang nzuri ambayo ni yenye mshikamano, mapatano, ustawi, na utamaduni wenye hali ya juu, mifumo bora ya ikolojia na watu wanaoishi na kufanya kazi kwa kuridhika, katika mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Rais Xi amefanya ziara Xinjiang baada ya kurejea China kutoka kwenye mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS na ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini.

Akitambua mafanikio ya Xinjiang katika nyanja mbalimbali, Rais Xi amesema kazi inayohusiana na Xinjiang ina umuhimu maalumu katika kazi ya CPC na serikali ya China kwa ujumla na inahusu kazi ya jumla ya kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa ya kisasa yenye nguvu katika mambo yote na kuhimiza Ustawishaji wa Taifa la China.

“Juhudi zinapaswa kufanywa siyo tu kushughulikia matatizo makubwa yanayokwamisha maendeleo na utulivu wa Xinjiang, lakini pia kufanya mipango ya muda mrefu ya kuhimiza kazi muhimu, za msingi na za muda mrefu za kwa ajili ya ustawi na utulivu wa kudumu katika eneo hilo” amesema Rais Xi.

Kudumisha utulivu wa kijamii ni jambo la kipaumbele, Rais Xi amesema, huku akihimiza kufanyika juhudi za kuratibu kazi ya kudumisha utulivu na kuendeleza maendeleo, mambo mawili ambayo yanategemeana katika kuhimizwa. Pia ametaka juhudi za kuimarisha utawala wa sheria ili kujenga msingi imara wa kisheria wa kudumu kwa ajili ya utulivu.

Rais Xi pia amesisitiza kuwa inapaswa kuboresha mfumo wa kuzuia na kupunguza hatari kubwa na hatari zinazoweza kutokea na mapambano dhidi ya ugaidi na makundi ya kujitenga pia yanapaswa kufanyika pamoja na kulinda amani kwa mujibu wa sheria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha