Huduma ya kivuko cha feri yafikia kikomo baada ya daraja kubwa kufunguliwa kwa matumizi ya umma Yibin, Kusini Magharibi mwa China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 29, 2023
Huduma ya kivuko cha feri yafikia kikomo baada ya daraja kubwa kufunguliwa kwa matumizi ya umma Yibin, Kusini Magharibi mwa China
Picha hii iliyopigwa Julai 1, 2023 ikimwonyesha Zhong Helin, baharia wa kivuko cha feri kinachounganisha miji midogo ya Nixi na Juexi ya Eneo la Xuzhou la Mji wa Yibin, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Hongjing)

Huduma ya kivuko cha feri ambacho kinaunganisha miji midogo ya Nixi na Juexi ya Eneo la Xuzhou la Mji wa Yibin katika Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China ilianza Mei 1992. Huduma hii ya kivuko imekuwa mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafiri kwa wakazi wa eneo hilo wanaoishi karibu na pande zote za Mto Minjiang.

Wakati ambapo daraja kubwa la Nixi Minjiang limefunguliwa kwa matumizi ya umma hapa siku ya Jumatatu, huduma ya kivuko hicho cha feri ambayo imedumu kwa miaka 31 pia imefikia kikomo siku hiyo. Ufunguzi wa daraja kubwa la Nixi Minjiang umevunja kikwazo cha usafiri kwa zaidi ya watu 450,000 wanaoishi karibu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha