Mkutano wa kukutanisha wadau wa ugavi na mahitaji kabla ya Maonyesho ya CIIE waanza Shenzhen, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2023
Mkutano wa kukutanisha wadau wa ugavi na mahitaji kabla ya Maonyesho ya CIIE waanza Shenzhen, China
Wakala wa manunuzi (Kulia) akifahamishwa kuhusu vyakula kutoka Ulaya Kaskazini kwenye mkutano wa kukutanisha wadau wa ugavi na mahitaji kabla ya Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji Nje bidhaa ya China (CIIE) huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Agosti 29, 2023. (Xinhua/Mao Siqian)

Mkutano wa kukutanisha wadau wa ugavi na mahitaji kabla ya Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji nje Bidhaa ya China (CIIE) umeanza mjini Shenzhen siku ya Jumanne, na kuweka jukwaa la mawasiliano kati ya kampuni zaidi ya 200 za Eneo la Ghuba ya Guangdong-Hong Kong-Macao na wafanyabiashara wapatao 60 kutoka Tasnia ya Teknolojia za Akili Bandia na Teknolojia ya Habari, Bidhaa za Chakula na Kilimo na Biashara ya Huduma ya CIIE.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha