Viongozi wakuu wa China wapongeza Mkutano Mkuu wa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2023
Viongozi wakuu wa China wapongeza Mkutano Mkuu wa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo
Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Xi Jinping akihudhuria hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo na jamaa zao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Agosti 31, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Mkutano Mkuu wa 11 wa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo na jamaa zao umefunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China siku ya Alhamisi asubuhi.

Viongozi wakuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Serikali ya China wakiwemo Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Han Zheng walishiriki kwenye hafla ya kufunguliwa kwa mkutano na kutoa pongezi zao. Li Xi alitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC.

Takriban wajumbe 1,200 wa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo na jamaa zao kutoka kote nchini China na karibu Wachina 600 wa ng'ambo kutoka zaidi ya nchi 100 walihudhuria mkutano huo.

Katika hotuba hiyo, Li Xi ametoa pongezi kwa mkutano huo na kutoa salamu kwa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo na jamaa zao, Wachina wa ng'ambo, na wafanyakazi wa Shirikisho la China Nzima la Wachina Waliorejea kutoka Ng'ambo (ACFROC).

Li ameipongeza ACFROC na mashirika tanzu kwa kutekeleza majukumu yao na kujiboresha katika miaka iliyopita tangu Mkutano Mkuu wa 10 ulipofanyika.

“Wachina waliorejea kutoka ng'ambo na jamaa zao na Wachina walioko ng'ambo sasa wametumia fursa zao za kipekee na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, kupunguza umaskini, mapambano dhidi ya UVIKO-19, ufunguaji mlango, ustawi na utulivu wa muda mrefu wa Hong Kong na Macao, na muungano wa Taifa la China” Li amesema.

Amesisitiza ulazima wa watu wote wa Taifa la China ndani na nje ya nchi kufanya juhudi za pamoja ili kutimiza Lengo la Pili la Miaka 100 la kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya mambo ya kisasa kwa pande zote na kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote kupitia Njia ya Maendeleo ya Mambo ya Kisasa ya China.

Watu wa mfano wa kuigwa miongoni mwa Wachina waliorejea kutoka ng'ambo na watu mashuhuri na vikundi chini ya ACFROC na mashirika yake tanzu walitunukiwa katika mkutano huo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha