China yajipanga kukabiliana na kimbunga kikali Saola kuelekea kuanza kwa muhula mpya wa masomo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2023
China yajipanga kukabiliana na kimbunga kikali Saola kuelekea kuanza kwa muhula mpya wa masomo
Boti zikijiandaa kuegesha ili kujilinda kwa usalama kwenye Kimbunga Saola kinachokaribia huko Quanzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Agosti 30, 2023. (Xinhua/Wei Peiquan)

GUANGZHOU/FUZHOU – Ili kukabiliana na kimbunga kikubwa Saola kinachokaribia, miji mingi katika mikoa ya pwani ya China, ikiwa ni pamoja na Guangdong na Fujian, imeahirisha kuanza kwa muhula mpya wa masomo, kusimamisha shughuli za treni na feri, na kuelekeza boti za uvuvi katika maeneo ya maji yaliyoathiriwa kurudi bandarini kwa ajili ya usalama.

Miji mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shantou, Shanwei, Jieyang na Chaozhou katika Mkoa wa Guangdong, Mashariki mwa China, na Quanzhou na Zhangzhou katika Mkoa wa Fujian imesogeza mbele muda wa kuanza kwa muhula mpya wa masomo hadi Septemba 4 kwa shule za msingi, sekondari na chekechea.

Utumiaji wa njia za reli za sehemu za Mkoa wa Guangdong, pamoja na njia ya kati ya Guangzhou-Shenzhen na njia ya reli ya mwendokasi ya Guangzhou-Shenzhen-Hong Kong, unatarajiwa kusimamishwa kutoka Alhamisi hadi Jumatatu, kwa mujibu wa Shirika la Reli la China, Tawi la Guangzhou.

Ili kukabiliana na kimbunga hicho, Makao Makuu ya Idara ya Mafuriko, Ukame na Udhibiti wa Vimbunga ya Mkoa wa Guangdong yamepandisha mwitikio wake wa dharura kwa Ngazi ya II saa 2 asubuhi siku ya Alhamisi.

Hatua kama hizo ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kwa shughuli za treni pia zimetekelezwa katika mkoa jirani wa Fujian.

Huko Shanwei, Guangdong, ambako huenda kimbunga hicho kitatua siku ya Ijumaa, makao makuu ya idara ya mafuriko, ukame na udhibiti wa vimbunga ya mji huo siku ya Alhamisi yaliamuru kusimamishwa kwa shughuli za shule, ujenzi, uzalishaji, usafirishaji na biashara kuanzia Ijumaa hadi pale tahadhari ya Ngazi ya I ya mwitikio wa dharura wa kimbunga itakapoondolewa.

Idara ya Taifa ya Uchunguzi wa Unajimu ya China siku ya Alhamisi ilihuisha tahadhari nyekundu kwa kimbunga Saola, ambayo ni tahadhari kali zaidi katika mfumo wake wa tahadhari kwa vimbunga wenye ngazi nne, wakati kimbunga hicho ambacho ni cha tisa kuikumba China katika mwaka huu kikitarajiwa kuleta upepo na mvua kubwa katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha