Jukwaa Jipya laimarisha ushirikiano kati ya jumuiya za vyuo vikuu vya China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2023
Jukwaa Jipya laimarisha ushirikiano kati ya jumuiya za vyuo vikuu vya China na Afrika
Picha iliyopigwa Agosti 31, 2023 ikionesha hafla ya uzinduzi wa Sekretarieti ya China ya Taasisi ya Mfumo wa Mabadilishano kati ya Vyuo Vikuu vya China na Afrika iliyofanyika hapa Beijing, China. (Picha/Kwa hisani ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing)

Jumuiya ya China ya Elimu ya Juu (CAHE) na Umoja wa Vyuo Vikuu vya Afrika (AAU) zimefanya hafla ya uzinduzi wa Sekretarieti ya China ya Taasisi ya Mfumo wa Mabadilishano kati ya Vyuo Vikuu vya China na Afrika katika Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) hapa Beijing, Agosti 31, 2023.

Rais wa CAHE, Du Yubo, anaona uzinduzi wa sekretarieti hiyo mpya kuwa fursa muhimu ya ushirikiano wa elimu ya juu wa China na Afrika, ambayo hakika itafungua mustakabali mpana zaidi wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Olusola Oyewole, Katibu Mkuu wa AAU amesema kuwa, vyuo vikuu vya China na Afrika vitatumia vizuri jukwaa hilo la Taasisi ya Mfumo wa Mabadilishano kati ya vyuo vikuu vya China na Afrika, ili kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya mabadilishano na ushirikiano wa elimu wa China na Afrika.

Mnamo mwezi wa Novemba, 2022, CAHE na AAU zilizindua uwenzi wa ushirikiano, ikiashirikia maamuzi ya Taasisi ya Mfumo wa Mabadilishano ya Vyuo Vikuu vya China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha