Hakuna mgongano wa maslahi kati ya China na Ulaya - Waziri Mkuu wa China Li Qiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2023
Hakuna mgongano wa maslahi kati ya China na Ulaya - Waziri Mkuu wa China Li Qiang
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Kundi la nchi 20 (G20) mjini New Delhi, India, Septemba 10, 2023. (Xinhua/Yao Dawei)

NEW DELHI - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema zikiwa katika ncha tofauti za Bara la Ulaya na Asia, Eurasia, hakuna mgogoro wa siasa za kijiografia kati ya China na Ulaya, achilia ambali mgongano wowote wa maslahi kati ya pande hizo mbili.

“China iko tayari kushirikiana na Ulaya ili kuhimiza maendeleo thabiti na yenye ustawi ya uhusiano wa pande hizo mbili,” Waziri Mkuu Li amesema siku ya Jumapili alipokutana na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Kundi la nchi 20 (G20).

Amesema, kwa vile China na Ulaya ni sehemu mbili zenye nguvu, masoko na ustaarabu duniani, uhusiano kati ya China na Ulaya unabeba utulivu wa kimataifa na ustawi wa Bara la Ulaya na Asia, Eurasia.

Ameongeza kuwa China inatarajia kuona Ulaya yenye ustawi na utulivu, iko tayari kushirikiana na upande wa Ulaya kuendelea kujitolea kwa ushirikiano wao, kuimarisha zaidi mazungumzo na mabadilishano, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, kushughulikia ipasavyo masuala nyeti, ili kukuza uhusiano wenye uendelevu, bora na thabiti kati ya China na Ulaya na kuingiza utulivu na nishati chanya katika Dunia hii yenye misukosuko.

Huku akisema mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Umoja wa Ulaya, Waziri Mkuu Li amesema maendeleo ya China ni fursa kwa Ulaya, si hatari, na pande zote mbili zinapaswa kuendelea kufungua mlango na kushirikiana kwa manufaa ya pande zote.

Haijalishi sasa au katika siku zijazo, Waziri Mkuu Li ameahidi kwamba China itaendelea kuwa rafiki na mshirika wa kuaminika wa Ulaya.

Kwa upande wake Michel, amesema kuwa EU iko tayari kuwa rafiki na mshirika wa dhati, wa kuaminika na wa kiujenzi wa China.

“China yenye ustawi mzuri ni manufaa kwa EU na Dunia nzima, na EU haina nia ya kuzuia maendeleo ya China,” Michel amesema huku akisisitiza kuwa EU inaheshimu na kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja na inataka kuimarisha mazungumzo na ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali, na kushughulikia kwa pamoja changamoto za kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi, afya ya umma, usalama na utulivu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha