Habari picha ya mwalimu wa elimu maalum katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2023
Habari picha ya mwalimu wa elimu maalum katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Fu Yaohui akifundisha somo darasani kwenye Shule ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum ya Hainan (Haikou) huko Haikou, Mkoa wa Hainan Kusini mwa China, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)

Fu Yaohui ni mwalimu katika shule ya elimu maalum huko Haikou. Tangu Mwaka 2004, Fu amekuwa akijishughulisha na elimu maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu wa akili, kukuza ujuzi wao wa kimsingi ili kuweza kuendana na maisha ya kila siku.

Kila siku, Fu hufika shuleni mapema na kuwasaidia wanafunzi kwa subira na kuwatia moyo. "Nataka wanafunzi wangu watajua kujitegemea ," amesema. Ili kufikia lengo hilo, anajitahidi kadiri awezavyo kuwasaidia watoto hao, ili waweze kufaulu masomo yao na kuwawezesha kujumuika vyema katika jamii. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha