Ushirikiano wa Eneo Maalum la Viwanda kati ya China na Indonesia waleta manufaa kwa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 12, 2023
Ushirikiano wa Eneo Maalum la Viwanda kati ya China na Indonesia waleta manufaa kwa pande mbili
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa uzalishaji na usindikaji vyakula vya baharini katika Kiwanda cha Kampuni ya Vyakula vya Majini ya Zhaohua huko Fuqing, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Agosti 24, 2023. (Xinhua/Zhou Yi)

FUZHOU - Katika shamba lililoko Wilaya ya Pemalang katika Jimbo la Java ya Kati nchini Indonesia, vibuu vya samaki kamba sasa vimefikisha umri wa mwezi mmoja na nusu. Mara vitakapofikisha umri wa miezi minne, vitafanyiwa usindikaji na kusafirishwa hadi Fuzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China, ulio umbali wa maili 2,000 za baharini.

Mzalishaji wa samaki kamba wa msimu Joni Setyawan ndiye anayesimamia shamba hilo. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 66 ana uzoefu wa takriban miongo minne katika ufugaji wa samaki kamba aina ya Vannamei. Tangu Mwaka 2021, amekuwa akifanya kazi na kampuni tanzu inayomilikiwa kikamilifu na Kampuni ya Vyakula vya Majini ya MiaoTianHui ya Fujian, ikijikita katika ufugaji na uzalishaji wa samaki kamba.

Shamba hilo katika Wilaya ya Pemalang linachukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba karibu 70,000. Samaki kamba wanaozalishwa hapa hufanyiwa usindikaji wa mwanzo kama vile kusafishwa, kukwanguliwa magamba na kufungashwa kwa kugandishwa kwenye kiwanda nchini Indonesia Baada ya hapo, meli zinazobeba bidhaa hizi za majini zitaanza safari ya takriban siku 20 kabla ya kuwasili katika Bandari ya Fuzhou.

Wakijulikana kwa maumbo yao ya kupendeza na wa kutafunika kirahisi, samaki kamba hawa ni maarufu sana katika soko la chakula nchini China.

Kampuni ya Vyakula vya Majini ya Zhaohua ya Fuqing pia imewekeza katika uzalishaji wa kamba aina ya Vannamei nchini Indonesia, huku shamba lake likiwa na ukubwa wa mita za mraba karibu milioni 4.

Kuweka vituo vya uvuvi nchini Indonesia siyo tu kumeongeza fursa za ajira kwa wenyeji lakini pia kumeongeza kipato cha wakaazi, amesema Chen Qing'an, mkuu wa kampuni tanzu ya Indonesia ya Kampuni ya Vyakula vya Majini ya MiaoTianHui ya Fujian, huku akibainisha kuwa kampuni hiyo tanzu imeajiri wafanyakazi wenyeji zaidi ya 300.

"Nilikuwa na mabwawa matatu ya samaki kamba, lakini sasa nasimamia jumla ya mabwawa 70 kwenye mashamba mawili. Mapato yangu ya kila mwezi yameongezeka na kuwa thabiti sana," amesema Joni Setyawan na kuongeza kuwa ameuza nchini China samaki kamba wa vannamei wenye uzito wa takriban tani 1,200 katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita.

Chini ya mradi wa "Nchi Mbili, Maeneo Maalum Mawili ya Viwanda” na uunganishaji wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China na Dira ya Indonesia ya Eneo la Kimataifa la Bahari, eneo hilo maalum la viwanda la China limeanzisha miradi 27 ya uwekezaji nchini humo yenye uwekezaji wenye thamani ya yuan bilioni 55.4 (kama dola za kimarekani bilioni 7.57) na miradi 18 ya biashara.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha