Wanandoa ambao ni Mtanzania na Mchina kutoka Xinjiang, China waendesha mkahawa katika Mji Mkongwe Kashgar

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 12, 2023
Wanandoa ambao ni Mtanzania na Mchina kutoka Xinjiang, China waendesha mkahawa katika Mji Mkongwe Kashgar
Hadiya Msham Abdulla (kushoto) akiimba huku mumewe Dilxat Tursun aliyebeba mtoto wao mchanga mbele ya Mkahawa wa Dili na Diya ulioko eneo la kivutio la mji mkongwe wa Kashgar huko Kashgar katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Septemba 7, 2023. (Xinhua/Lan Hongguang)

Miaka saba imepita, Dilxat Tursun bado anaweza kuhisi moyo wake ukidunda kila anapokumbuka wakati aliposhika waridi 99 mkononi mwake na kukiri hisia zake kwa Hadiya Msham Abdulla kutoka Tanzania.

Ingawa Hadiya hakutoa jibu lake mara moja, wawili hao kwa sasa wako kwenye ndoa yenye furaha, wakiendesha Mgahawa wa Dili na Diya huko Kashgar, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China.

Mwaka 2012, Hadiya alikuja China na kusoma udaktari katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Fujian katika Mji wa Fuzhou.

Dilxat aliondoka nyumbani kwao Xinjiang kwenda chuo kikuu katika mji huo wa Fuzhou Mwaka 2013, hakujua kwamba alikuwa karibu kukutana na mpendwa wa maisha yake miaka mitatu baadaye.

Mwaka 2020, walioana baada ya miaka ya kuwa wapenzi. Miaka miwili baadaye, Hadiya aliamua kuambatana na mumewe hadi maskani yake ya Kashgar na akafungua mkahawa hapa.

Wanandoa hao walimimina mioyo na roho zao katika kuandaa kahawa bora zaidi. Mkahawa wa Dili na Diya umekuwa mahali maarufu katika eneo la mji wa Kashgar. Pia wanashiriki biashara na maisha yao ya kila siku kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii.

"Miaka ya hivi karibuni imeshuhudia maendeleo ya kasi hapa Kashgar. Eneo la mji mkongwe ni eneo lenye mandhari na uwezo mkubwa. Nina matumaini makubwa kuhusu eneo hili," amesema Dilxat. "Kuna nyumba ya chai yenye historia ya karne moja hapa Kashgar. Ninatumai kwamba katika siku zijazo mji huu utakuwa na mkahawa wenye historia ya karne moja-- mkahawa wetu."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha