

Lugha Nyingine
Hafla ya kutunuku washindi wa Tuzo ya Tatu ya "China ya maajabu katika kamera - Mashindano ya Upigaji picha kuhusu China katika Macho ya Wajapani" yafanyika Tokyo (3)
Hafla ya kutunuku washindi wa Tuzo ya Tatu ya "China ya maajabu katika kamera - Mashindano ya Upigaji picha kuhusu China katika Macho ya Wajapani" imefanyika kwenye Kituo cha Utamaduni cha China huko Tokyo, Japan Septemba 6.
Watu zaidi ya 120 wa China na Japan kutoka sekta mbalimbali wakiwemo Balozi wa China nchini Japan Wu Jianghao, Konsela wa Utamaduni wa Ubalozi wa China nchini Japan Chen Zheng, Konsela wa Habari na Diplomasia ya Umma wa Ubalozi wa China nchini Japan Zhang Peilin, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Gazeti la Mtandaoni la People's Daily Tang Weihong, na Waziri Mkuu wa zamani wa Japani Yukio Hatoyama na wengineo walihudhuria hafla hiyo.
Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Yasuo Fukuda na Mwenyekiti wa shirikisho la Wapiga Picha la China, Li Ge wametoa salamu zao za pongezi na kheri kwa njia ya video, wakieleza mchango wa mashindano hayo katika kukuza mabadilishano ya watu kati ya China na Japan na kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Balozi Wu amesema katika hotuba yake kwamba mashindano hayo ni jukwaa muhimu kwa watu wa Japan kubadilishana maoni na maarifa yao kuhusu China. Amesema, kila picha inawakilisha kila "wakati mzuri wa China”, na mfululizo wa picha unaonyesha "simulizi ya China". "Simulizi ya China" ya kusisimua zaidi inayoendelea nchini China leo inaitwa "maendeleo ya kisasa ya mtindo wa China."
Amesema "Maendeleo ya kisasa ya mtindo wa China" yamejitolea kukuza maendeleo yenye ubora wa juu na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na yataleta fursa za ushirikiano kwa nchi kote duniani, pamoja na Japan.
Kwa upande wake Tang amesema kwamba mabadilishano ya kitamaduni na utalii ni moja ya njia muhimu za mawasiliano yasiyo ya kiserikali kati ya China na Japan.
Amesema, washiriki wa mashindano ya tuzo hiyo wametumia lenzi zao kurekodi maeneo ya vivutio vya China, mandhari ya asili, desturi za kikabila, na maisha ya watu katika mitaa. “Tumehisi urafiki na nia njema ya watalii wa Japan juu ya China, na pia tumeona uzuri wa China kwa njia ya kipekee” amesema.
Shughuli za mashindano ya Tuzo ya Tatu ya "China ya maajabu katika kamera - Mashindano ya Upigaji picha kuhusu China katika Macho ya Wajapani" yaliandaliwa na Ubalozi wa China nchini Japan.
Tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2016, yamefanyika kwa mafanikio mara tatu. Katikati ya Novemba 2022, Mashindano hayo ya tuzo ya tatu, yenye mada ya maadhimisho ya kutimia miaka 50 tangu kurejeshwa kawaida kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Japan na kukaribisha maadhimisho ya kutimia miaka 45 tangu kutiwa saini Mkataba wa Amani na Urafiki kati ya China na Japan ya Mwaka 2023, yalifunguliwa rasmi.
Baada ya uteuzi wa awali wa jopo la majaji na mapitio ya wataalam wa tasnia za upigaji picha za China na Japan, katika mashindano ya tuzo hiyo, kazi 7 zilizoshinda tuzo zikiwemo tuzo maalum hatimaye zilichaguliwa, na pia kulikuwa na "Tuzo ya Usafiri wa Anga wa Kimataifa wa China" na "Tuzo ya People’s Daily“.
Katika hafla hiyo ya tuzo, wawakilishi kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo walitoa tuzo kwa washindi na kutoa maoni ya kitaalamu juu ya kazi zilizoshinda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma