

Lugha Nyingine
Ushirikiano wa nishati safi kando ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja waleta nuru Asia ya Kati (8)
![]() |
Picha hii iliyopigwa Agosti 14, 2022 ikionyesha mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 50 kwa upepo huko Kostanay, Kazakhstan. (Xinhua) |
SHANGHAI/ALMATY - Akipambana na jua kali, mhandisi Rinat Turganbekov alikuwa akishika doria kupita safu zinazonga’ra za paneli za kuzalisha umeme kwa nishati ya jua zinazopamba nyanda pana za Kazakhstan.
Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua cha Kapshagay, mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika nchi hiyo ya Asia ya Kati, ni sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nishati safi kati ya China na Kazakhstan, uliowekezwa kwa pamoja na kujengwa na kampuni ya Nishati ya Universal ya China na wabia wake wa Kazakhstan.
Akiwa ni mfanyakazi wa muda mrefu wa Kampuni ya Nishati ya Universal Tawi la Kazakhstan, Turganbekov ameshuhudia mabadiliko ya ajabu yaliyoletwa na vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua, na kuwapa wakazi wa eneo hilo umeme wa safi na wa bei nafuu.
Wakati huo huo, kando ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, mfululizo wa juhudi za ushirikiano zinazolenga maendeleo endelevu zinaandika ukurasa mpya wa ushirikiano wa kunufaishana.
"Kampuni za China zimeleta mabadiliko makubwa katika maisha yangu," amesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye alisoma Tianjin, China na anaongea vizuri Lugha ya Kichina.
Hapo awali, alifanya kazi kama mkarimani katika kampuni hiyo. Wakati alipofanya kazi hiyo, wafanyakazi wenzake wa China walimtia moyo kujitosa katika uratibu wa mradi.
Katika miaka yake mitano ya kufanya kazi na kampuni hiyo, Turganbekov ameshiriki katika miradi kadhaa ya ujenzi. Mwaka 2020, mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua cha Kaskelen, kilichojumuishwa kwenye orodha ya miradi muhimu ya ushirikiano wa uwezo wa uzalishaji na uwekezaji kati ya China na Kazakhstan, ulikuwa katika hatua muhimu.
Kwa juhudi za pamoja za timu za China na Kazakhstan, kituo hicho cha kuzalisha umeme cha Kaskelen kiliunganishwa kwa mafanikio kwenye gridi ya taifa na kuanza kuzalisha umeme Juni 2020, kikizalisha umeme kilowati milioni 80.8 kwa saa kila mwaka na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni wa Kazakhstan kwa tani 80,800.
Nishati safi siyo tu imewezesha Kazakhstan kuhama kuelekea maendeleo endelevu lakini pia huwapa wakazi wake upatikanaji wa umeme wa gharama nafuu.
Nan Yi, mwenyekiti wa kampuni hiyo ya nishati ya China, amebainisha kuwa tangu Mwaka 2015, kampuni yake imekuwa ikiwekeza katika miradi ya nishati mpya nchini Kazakhstan, ikiwa ni pamoja na vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati za jua na upepo. Hadi sasa, imekamilisha ujenzi wa vituo sita vipya vya nishati vyenye uwezo wa kuzalisha umeme megawati 380, vyote vimeorodheshwa kwenye orodha ya miradi muhimu ya ushirikiano wa uwezo wa uzalishaji na uwekezaji kati ya China na Kazakhstan.
Miradi hii inapunguza utoaji wa hewa ya kaboni kwa tani milioni moja kila mwaka, huku ikikidhi mahitaji ya umeme ya takriban kaya 600,000 za wenyeji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma