Mashindano ya Kimataifa ya Simulizi ya “Majaaliwa yangu na Lugha ya Kichina” ya Mwaka 2023 yahitimishwa kwa Mafanikio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2023
Mashindano ya Kimataifa ya Simulizi ya “Majaaliwa yangu na Lugha ya Kichina” ya Mwaka 2023 yahitimishwa kwa Mafanikio
Li Xikui, naibu mkuu wa wa Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa nchi za nje akitoa hotuba. (Picha na Lu Pengyu, Gazeti la Mtandaoni la People's Daily)

Fainali za Mashindano ya Kimataifa ya Simulizi ya “Majaaliwa yangu na Lugha ya Kichina” ya Mwaka 2023, yanayoandaliwa kila mwaka na Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa Nchi za Nje na kuendeshwa na Gazeti la Mtandaoni la People's Daily, Kamati ya Chama ya Jincheng, Serikali ya Mji wa Jincheng na Kundi la Kampuni za Shanxi Huangcheng Xiangfu, zimehitimishwa kwa mafanikio Alhamisi ya Septemba 14 huko Jincheng, Mkoa wa Shanxi, China.

Vikundi kumi vya washiriki kutoka Poland, Kenya, Pakistani, Chad, Nigeria, Ghana, Laos, Sudan, Mongolia, na Russia walitoa masimulizi mazuri ya moja kwa moja jukwaani yenye mada ya “Maskani”.

Li Xikui, naibu mkuu wa Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa Nchi za Nje, amesema katika hotuba yake: "Maandishi ya Kichina ni jeni ya ustaarabu wa China, mzizi wa utamaduni wa China, na daraja la kufanya mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu wa China na wa Dunia. Historia ya maendeleo ya binadamu ni hadithi ya mwingiliano wa ustaarabu mbalimbali. Ni kwa kuchota virutubisho kutoka kwa ustaarabu mbalimbali tofauti na kujifunza kutoka kwa nguvu za kila mmoja ndipo anga nyota ya ustaarabu wa binadamu inaweza kung'aa zaidi na maskani ya pamoja ya binadamu kuwa na amani na ustawi. "

Tang Weihong, Mjumbe wa Kamati ya Chama na Mwenyekiti wa Bodi ya Wasimamizi wa Gazeti la Mtandaoni la People's Daily amesema katika hotuba yake: "Katika miaka kumi iliyopita, chini ya mfumo wa 'Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja', China na nchi nyingine kwa pamoja zimeandika ukurasa mzuri wa ushirikiano wa amani, wenye uwazi na jumuishi, kufundishana na kunufaishana. Binadamu ni Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja inayochangia shida na raha, Dunia ni maskani yetu ya pamoja. Dhana ya ‘maskani’imekita mizizi ndani ya vinasaba vya ustaarabu wa China."

Kwenye fainali za mashindano hayo, majaji walitathmini washiriki kulingana na uwezo wao wa kujieleza kwa Lugha ya Kichina, mguso wao wa jukwaani, na maadili ya msingi yaliyofafanuliwa kwenye simulizi. Mshiriki Li Haorui kutoka Nigeria hatimaye ameteuliwa kushinda taji na zawadi maalum; Sejoud Isam Mahir Hassan (Sudan) na Lydia Nduta Njoroge (Kenya) wameshinda nafasi ya kwanza ya tuzo ; Kaleem Sajid (Pakistani), Moses Arthur Baidoo (Ghana), Yasser Mahamad Senoussi+Ousama Mahamad Senoussi Ahmad (mapacha wa Chad) wameshinda nafasi ya pili ya tuzo; Siniakov Andrei (Russia), Senyord Chanmaly (Laos), Oyungerel Gegee (Mongolia), na Ratajczak Paulina Magdalena (Poland) wameshinda nafasi ya tatu ya tuzo.

Tangu mashindano hayo yatangazwe kuanza Mwezi Juni mwaka huu, yamevutia washiriki zaidi ya 3,000 kutoka nchi zaidi ya 70 duniani. Marafiki wa nchi mbalimbali na wa utamaduni tofauti waliungana kwenye maandishi ya Lugha ya Kichina na kusimulia simulizi kuhusu “maskini” mioyoni mwao. Baada ya raundi mbili za mashindano makali katika raundi ya awali na ile ya nusu fainali, makundi 10 ya washiriki yalijitokeza na hatimaye kukusanyika katika Mji wa Jincheng ulioko Shanxi, China kushindana kwenye hatua ya fainali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha