Kongamano lafanyika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Algeria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2023
Kongamano lafanyika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Algeria
Watu wakihudhuria Kongamano la Uchumi la China na Algeria mjini Oran, Algeria, Septemba 13, 2023.

ALGIERS - Maafisa waandamizi na wawakilishi wa biashara kutoka China na Algeria walikusanyika Jumatano katika bandari ya Oran Magharibi mwa Algeria kuhudhuria Kongamano la Uchumi la China na Algeria.

Kongamano hilo lililoandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Algeria na serikali ya Jimbo la Oran, Algeria limehudhuriwa na washiriki 200, wakiwemo wabunge wa Algeria na maafisa wa serikali pamoja na wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kongamano hilo, Balozi wa China nchini Algeria Li Jian amesema kongamano hilo linalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili kwa kuunda jukwaa la kurahisisha mawasiliano kati ya wafanyabiashara wa China na Algeria.

Gavana wa Jimbo la Oran Said Saayoud amesema uwekezaji wa China unakaribishwa katika jimbo lake na sheria mpya ya uwekezaji ya Algeria itawapa wawekezaji wa kigeni mazingira mazuri.

Kwenye kongamano hilo, mijadala mitatu ilifanyika kwa viongozi wa biashara kutoka sekta za ujenzi, mavazi na mawasiliano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha