Misitu ya kale ya chai katika eneo la Pu'er la China yaorodheshwa kuwa eneo la urithi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2023
Misitu ya kale ya chai katika eneo la Pu'er la China yaorodheshwa kuwa eneo la urithi wa Dunia
Picha hii iliyopigwa Agosti 29, 2023 ikionyesha kijiji cha jadi kilichozungukwa na misitu na mashamba ya chai kwenye Mlima Jingmai huko Pu'er, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Li He)

RIYADH - Mandhari ya Kitamaduni ya Misitu ya Chai ya Kale ya Mlima Jingmai katika Mji wa Pu'er, Kusini-Magharibi mwa China, ambayo ina misitu mitano mikubwa ya chai iliyohifadhiwa vizuri, vijiji tisa vya jadi pamoja na hifadhi za misitu mitatu, inasimama kama mfano wa utamaduni tajiri wa chai unaohusisha mila na desturi za kale za kulima na kuhifadhi misitu ya kale ya chai. Mandhari hiyo imeorodheshwa kwenye Orodha ya Mali ya Urithi ya Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) siku ya Jumapili.

Katika mkutano wake wa 45 ulioongezwa muda ambao unaendelea Riyadh, Saudi Arabia, Kamati ya Mali ya Urithi ya Dunia ya UNESCO imechunguza eneo hilo lililoteuliwa na China na kuliongeza kwenye orodha ya kuwa mali ya kitamaduni, na kulifanya kuwa eneo la 57 la China la Mali ya Urithi ya Dunia.

Uamuzi huo unaashiria uhai mkubwa unaodumu hivi leo wa misitu ya kale ya chai na mandhari ya kitamaduni inayohusika katika Mlima Jingmai ulioko Eneo linalojiendesha la Kabila la wa-Lahu la Lancang katika Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, mojawapo ya mikoa ambayo ilitumia rasilimali za chai mapema zaidi na kuwa na ushawishi mkubwa kwa utamaduni wa chai duniani.

Misitu imesimamiwa vizuri chini ya mfumo wa kipekee wa uhifadhi ambao unaheshimu tofauti za kitamaduni na kibaiolojia na matumizi endelevu ya maliasili, ambayo inaunganisha usimamizi wa serikali na ule wa ngazi ya chini, uliojengwa juu ya msingi wa imani za mababu juu ya chai za jadi .

Mfumo huu unaheshimu mazingira ya tabianchi ya eneo husika, sifa za topografia, na uwepo wa mimea na wanyama, kufikia uhifadhi wa viumbe na utamaduni anuai na matumizi endelevu ya maliasili.

"Kuwekwa kwenye orodha ya UNESCO kunaonyesha umuhimu wa nafasi ya China katika kuzaliwa kwa chai, kupandwa na kufanya biashara ya chai na uenezaji wa utamaduni wa chai duniani," Li Qun, Mkuu wa Idara ya Mali ya Kitaifa ya Urithi wa Utamaduni ya China, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye mkutano huo wa UNESCO.

Karibu katika karne ya 10, mababu wa kabila la Wabulang walihamia Mlima Jingmai, ambako waligundua na kujenga ujuzi juu ya miti ya chai ya mwitu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha