Uhusiano kati ya China na ASEAN ni mfano wenye mafanikio na nguvu zaidi katika ushirikiano wa Asia Pasifiki: Waziri Mkuu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2023
Uhusiano kati ya China na ASEAN ni mfano wenye mafanikio na nguvu zaidi katika ushirikiano wa Asia Pasifiki: Waziri Mkuu wa China
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya 20 ya China na nchi Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na Mkutano wa 20 wa Kilele wa Biashara na Uwekezaji wa China na ASEAN huko Nanning, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Septemba 17, 2023. (Xinhua/Yao Dawei)

NANNING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema kuwa uhusiano kati ya China na Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) umekuwa mfano wenye mafanikio na nguvu zaidi katika ushirikiano wa kikanda wa Eneo la Asia na Pasifiki, na mfano wazi wa jinsi ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa wote.

Waziri Mkuu Li ameyasema hayo siku ya Jumapili kwenye hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya 20 ya China na Umoja wa Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na Mkutano wa 20 wa Kilele wa Biashara na Uwekezaji wa China na ASEAN huko Nanning, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China

Amesema Maonyesho ya China na ASEAN yameshuhudia maendeleo endelevu ya uhusiano wa pande mbili tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, na pande hizo mbili zimejizatiti kujiimarisha kwa njia ya umoja, ushirikiano wa kunufaishana na kutilia maanani Dunia.

"Uhusiano mzuri kati ya China na ASEAN haupatikani kirahisi na ni matokeo ya juhudi za pamoja za pande zote," Waziri Mkuu Li amesisitiza, huku akibainisha kuwa msingi wa uhusiano huo ni upendo, ukweli, ujumuishaji na kutilia mkazo kufikia manufaa ya pande zote.

Ametoa wito wa kufanyika juhudi za kuweka mazingira mazuri yatakayoleta maendeleo, ustawi, amani na utulivu, ili maendeleo ya nchi moja yaweze kunufaisha zaidi nchi jirani na watu wa eneo hilo.

Amesema China iko tayari kupanua ushirikiano na ASEAN katika nyanja kama vile utamaduni, utalii, mafunzo na vijana ili kuongeza maelewano na urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili, na hivyo kuzidisha muunganisho wa kihisia.

Takriban watu 1,200 wamehudhuria hafla hiyo ya ufunguzi, wakiwemo Waziri Mkuu wa Cambodia, Hun Manet, Waziri Mkuu Laos Sonexay Siphandone, Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, Waziri Mkuu wa Vietnam, Pham Minh Chinh, Makamu wa Rais wa Indonesia Ma'ruf Amin, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Biashara wa Thailand, Phumtham Wechayachai na Katibu Mkuu wa ASEAN Kao Kim Hourn, pamoja na wawakilishi wa kibiashara kutoka China, ASEAN, na nchi na maeneo mengine.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha