Shirikisho la Watu wenye Ulemavu la China lafanya mkutano mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2023
Shirikisho la Watu wenye Ulemavu la China lafanya mkutano mkuu
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akisalimiana na wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa nane wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 18, 2023. Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu la China limefungua mkutano wake mkuu wa nane wa kitaifa mjini Beijing siku ya Jumatatu. (Xinhua/Pang Xinglei)

Beijing – Mkutano mkuu wa 4 wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu la China limefunguliwa siku ya Jumatatu hapa Beijing, ambapo Rais Xi Jinping, na viongozi wengine wa CPC na serikali ya China walihudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa pongezi.

Naibu Waziri Mkuu wa China, Ding Xuexiang ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) alitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na Baraza la Serikali la China.

Katika hotuba yake, Ding amesema mambo ya watu wenye ulemavu wa China yamekuwa yakiendelezwa katika hali motomoto chini ya uongozi thabiti wa Kamati Kuu ya CPC na Komredi Xi Jinping akiwa katibu mkuu wake.

Amesema China imefikia kwa muda uliopangwa lengo la kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote na hakuna hata mtu mmoja mwenye ulemavu anayeachwa nyuma.

Amesisitiza juhudi za kutekeleza kikamilifu kauli na maagizo muhimu ya Rais Xi, kutilia maanani maadili ya usawa, ujumuishaji na kunufaika pamoja, na kujikita katika kazi ya kuendeleza ustawi wa pamoja kati ya watu wenye ulemavu, na kuhimiza maendeleo ya pande zote ya miradi ya watu wenye ulemavu.

Ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kujenga maisha bora na yenye furaha kwa watu wenye ulemavu katika mchakato wa kuleta maendeleo ya kisasa ya China.

Zhang Haidi, Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu la China, alitoa ripoti ya kazi katika mkutano huo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha