Urafiki thabiti kati ya China na Zambia waleta manufaa halisi kwa watu wa Zambia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2023
Urafiki thabiti kati ya China na Zambia waleta manufaa halisi kwa watu wa Zambia
Wanawake wa Zambia wakicheza ngoma kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa barabara kuu uliofadhiliwa na China huko Chisamba, Zambia, Septemba 8, 2017. (Xinhua/Peng Lijun)

LUSAKA - Kwa Fidelity Sindolo, ambaye anaendesha saluni ya nywele katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, kukatika kwa umeme kulikuwa kukiumiza sana kichwa chake, na kuifanya biashara yake ikatike mara kwa mara.

Mwezi Machi mwaka huu, Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Maji cha Bwawa la Kafue kilichojengwa na China, kilichoko kilomita karibu 90 Kusini mwa Lusaka, kilianza kutumika, na kuzalisha umeme thabiti ambao unawezesha maisha na kustawisha shughuli za kiuchumi za wakazi wa eneo hilo.

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ambaye alizindua rasmi mradi huo, alisema kukamilika kwake siyo tu kunasaidia sekta ya nishati bali pia uchumi wa nchi hiyo kwa ujumla kwani nishati ni muhimu katika kuendesha uchumi.

Wiki iliyopita, kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China, Rais Hichilema alifanya ziara ya kiserikali nchini China. Viongozi hao wawili walitangaza kupandisha uhusiano wa pande mbili hadi kuwa na ushirikiano wenzi wa kimkakati wa pande zote, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wao wa kirafiki wa jadi.

Urafiki wa kudumu

China na Zambia zina urafiki wa kudumu na wa jadi, ambao ulijengwa na viongozi wa nchi hizo mbili za vizazi vilivyopita. Mapema katika miaka ya 1960, watu wa China waliunga mkono kwa dhati watu wa Zambia katika kutafuta uhuru wa kitaifa. Zambia ilikuwa nchi ya kwanza ya Kusini mwa Afrika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China.

Katika miaka ya 1970, kwa ombi la Tanzania na Zambia, China ilijenga Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), ijulikanayo kwa jina la Njia ya Urafiki na Njia ya Uhuru, kwenye nyanda kubwa za Afrika. Baadhi ya wahandisi na wafanyakazi walifariki dunia kwenye ujenzi wa mradi huo.

Ushirikiano mkubwa zaidi

Kituo cha kuzalisha umeme cha Kafue ni ushuhuda wa ushirikiano wa karibu kati ya China na Zambia. Katika miaka ya hivi karibuni, China na Zambia zimekuwa na ushirikiano wa pande zote ndani ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

China na Zambia kwa pamoja zimejenga miradi mingi ya maendeleo kama vile jengo jipya la kisasa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Simon Mwansa Kapwepwe, mitambo ya kisasa ya kusaga nafaka, mradi wa usambazaji maji wa Kafue na mingine mingi.

Mwaka 2022, China na Zambia zilitia saini makubaliano ya kuuza stevia na unga wa soya kwenye soko la China, na China iliamua kutotoza ushuru kwa 98% bidhaa za Zambia zinazoingia soko la China. Mwaka 2022, thamani ya kiwango cha biashara kati ya China na Zambia ilifikia dola za kimarekani bilioni 6.73, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30.2 kuliko mwaka uliopita wakati kama huo, ambalo ni la juu zaidi katika historia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha