Wasanifu majengo kutoka China wasanifu Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha DRC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2023
Wasanifu majengo kutoka China wasanifu Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha DRC
Picha iliyopigwa tarehe 25, Agosti ikionesha hali ya ujenzi wa Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Afrika ya Kati huko Kinshasa, mji mkuu wa DRC. (Picha ilipigwa na Shi Yu/Shirika la Habari la China Xinhua.)

Kwenye Barabara ya Triumph ya Kinshasa, Mji Mkuu wa Jamhuri ya Kango ya Kidemorasia (DRC), kuna majengo maarufu ya Ikulu ya Umma na Uwanja wa Mashujaa yaliyojengwa chini ya msaada wa watu wa China miaka ya 1970 na 1980. Kuvuka upande mwingine wa barabara hiyo, jengo jipya kabisa, Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Afrika ya Kati, kinaendelea kujengwa.

“Ikulu ya Umma ni makao ya Bunge la DRC, na Uwanja wa Mashujaa wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 hutumika kufanya shughuli muhimu,” amesema Alexis Gizaro Muvuni, Waziri wa Nchi na Waziri wa Miundombinu na Ujenzi wa DRC, akiongeza kuwa Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Afrika ya Kati ni “kadi nyingine nzuri ya utambulisho wa ushirikiano kati ya DRC na China.”

Taasisi ya Usanifu wa Majengo iliyosanifu kituo hicho ina makao makuu yake kwenye Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei wa China. Msanifu Mkuu wa mradi huo Tang Wensheng amesema, “Baba yangu aliwahi kufanya kazi na kuishi barani Afrika. Nimekuwa nikiipenda Afrika, tangu nikiwa mtoto. Mara tu niliposikia mradi huu upo Afrika, nilitamani kujaribu.”

Sehemu kuu ya jengo hilo inaundwa na Kituo cha Utamaduni pamoja na Chuo cha Sanaa cha Taifa cha DRC, ikiwa ni pamoja na jumba kubwa la sanaa za jukwaani lenye kuchukua watu 2,000 wakiwa wamekaa kwenye viti, jumba dogo la michezo ya jukwaani lenye kuchukua watu 800 wakiwa wamekaa kwenye viti, na Chuo cha Sanaa cha Taifa cha DRC kinachoweza kuchukua wanafunzi 2,000.

Dhana ya kuendana na mazingira halisi ya DRC inaonekana kwenye hatua mbalimbali za usanifu na ujenzi wa kituo hicho. Wasanifu wametumia mtindo wa jadi wa ua wa China ili kufanya mpangilio wa majengo ya shule ufae hali ya hewa ya nchi hiyo.

Baada ya kituo hicho kukamilika, walimu na wanafunzi wa Chuo cha Sanaa cha Taifa cha DRC watahamia kwenye chuo hicho kipya kusoma masomo na kufanya kazi. Wakati huo huo, wataweza kuonesha ujuzi wanaosoma na matunda ya ubunifu kwa dunia nzima kwenye jumba la michezo ya jukwaani la kituo hicho.

“Sote tunatamani kuhamia kwenye majengo haya mazuri,” amesema mwalimu mkuu wa Chuo cha Sanaa cha Taifa cha DRC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha